SERIKALI, UN, VYOMBO VYA HABARI KUTOA ELIMU DHIDI YA EBOLA – Mwanaharakati Mzalendo
ADVERTISEMENT
  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Mwanaharakati Mzalendo
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
No Result
View All Result
Home ELIMU

SERIKALI, UN, VYOMBO VYA HABARI KUTOA ELIMU DHIDI YA EBOLA

I am Magnifico by I am Magnifico
Nov 13, 2014
in ELIMU
0 0
0
0
SHARES
36
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter
001
ADVERTISEMENT
Mkurugenzi Msaidizi Kitengo cha Elimu ya Afya kwa Umma kutoka Wizara ya Afya na Ustawi ya Jamii, Said Makora (kulia), akielezea jinsi Wizara hiyo inavyopambana kutoa elimu ya ugonjwa wa Ebola kwa wananchi wakati wa kongamano lililoandaliwa na UNESCO, WHO, UNICEF, Wizara ya Afya na Ustawi ya Jamii, uliofanyika katika ukumbi wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT), Novemba 11,2014 jijini Dar es Salaam mkutano huo uliowakutanisha wamiliki wa Redio za kijamii kuwaelimsha Radio za Kijamii za Mikoani ni namna gani wanavyoweza kushirikiana na Wizara ya Afya na Ustawi ya jamii ili kutoa taarifa sahihi kwa wananchi kuhusu ugonjwa wa Ebola, Ebola ni nini namna ya kujinga na dalili zake.(kushoto), Kushoto ni Mwenyekiti wa COMNETA ambaye pia ni Mkurugenzi wa Redio FADECO, Sekiku Joseph.(PICHA NA PHILEMON SOLOMON).
Na Mwandishi wetu
SERIKALI , Mashirika ya Umoja wa Mataifa (UN) na vyombo vya habari nchini hapa vimekubaliana kufanyakazi kwa pamoja kwa ajili ya kuelimisha watanzania kuhusu ugonjwa hatari wa Ebola.
Katika juhudi za kuwekana sawa kuhusu uelimishaji wa umma kuhusu ugonjwa huo, kumefanyika kongamano la mafunzo kwa siku mbili, Chuo Kikuu huria jijini Dar es salaam.Kongamano hilo lilifanyika Novemba 10 na 11.
Kongamano hilo liliwashirikisha viongozi wa radio za wananchi zaidi ya 28 kutoka Visiwani na Tanzania Bara.
Katika kongmano hilo kulitengenezwa mikakati mbalimbali yenye kuleta uelewa kwa umma na kuwafanya kuchukua hatua za tahadhari na kuzuia ugonjwa huo usiingie nchini.
002
Mshauri wa Redio Jamii na Mkufunzi kutoka Shirika la Kimataifa la Elimu Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Bi. Rose Mwalimu akiendesha majadiliano kuhusu mikakati endelevu itakayowezesha kuihusisha jamii katika upatikanaji wa taarifa sahihi juu ya ugonjwa wa Ebola wakati wa kongamano hilo lililowakutanisha wamiliki wa radio za kijamii lengo ni kuwaelimsha Radio za Kijamii za Mikoani ili kutoa taarifa zilizo sahihi kwa wananchi kuhusu ugonjwa wa Ebola.
Kwa mujibu wa mmoja wa watu wanaounda kikundi kazi chenye lengo la kukabiliana na ugonjwa huo mafunzo hayo yaliandaliwa na Shirika la sayansi, elimu na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO) .
Aidha mafunzo hayo yaliwezeshwa kwa pamoja kati ya wizara ya afya na Umoja wa Afya duniani (WHO), na Shirika la kusaidia watoto la UNICEF.
Mafunzo hayo yaliyokuwa na washiriki walikuwa ni pamoja na wanachama wa wanamtandao wa vyombo vya habari Tanzania (COMNETA), yaligusa zaidi redio ambapo 25 kati yake zinaohudumiwa na Umoja wa Mataifa.
Wakati lengo kuu ni kuwafanya watanzania waujue ugonjwa huo na kuanza kuchukua hatua za tahadhari, mafunzo yalilenga kushawishi vyombo hivyo kutenga muda mchache kwa ajili ya elimu hiyo ili kuzuia mlipuko wake nchini.
003
Mkurugenzi wa Redio Kwizera ilioko Ngara-Kagera, Damas Missanga akichangia mada yake wakati wa kongamano la kuwaelimsha wamiliki wa Redio za Kijamii za Mikoani ili kutoa taarifa zilizo sahihi kwa wananchi kuhusu ugonjwa wa Ebola.
Katika mafunzo hayo washiriki walidadavua ebola nini na jamii inaweza kujijenga namna gani ili kukabiliana na janga hilo la kidunia.
Matumizi ya elimu ya mawasiliano yalitiliwa mkazo hasa kwa kubaini kwamba elimu hiyo ndiyo itakayoweza kutengeneza mkakati wa kuwabadili wengine na hivyo kuzuia kuingia kwake na kusambaa.
Washiriki na wawezeshaji walikubali kufanyakazi ya pamoja na Tume ya taifa inayoratibu mapambano dhidi ya Ebola katika kuelimisha umma kwa kuweka wazi taarifa za ugonjwa huo na namna ya kukabiliana nao.
Iliamuriwa kwamba radio hizo za jamii zitatumika kuanzisha midahalo yenye lengo la kuwasilisha taarifa mbalimbali kutoka kwa kikosi kazi cha kukabiliana na ugonjwa huo.
004
Meneja wa Redio jamii FADECO ya wilayani Karagwe, Adelina Lweramula akichangia mada wakati wa kongamani hilo.
Radio hizo ambazo zina changamoto ya aina yake kuanzia zile za wafugaji wa Serengeti ambako mara nyingi nyama ndizo zinazoliwa hadi kwenye jamii mbalimbali na hasa makorido yenye wageni wengi kama Zanzibar.
Aidha kongamano hilo limeboresha ushirikiano kati ya vyombo vya habari na serikali za mitaa ili kuendelea kutoa taarifa sahihi na zinazozingatia utamaduni wa eneo husika huku kukiwa na wito wa mabadiliko.
Katika kukabiliana na janga la Ebola na virusi vya Marburg, mafunzo hayo yaliangalia pia umuhimu wa kushirikiana katika kuhakikisha kwamba ugonjwa huo unashughulikiwa na kila mtu na kuondokana na hofu zinazofanya watu wayakimbie maeneo husika.
Kumeelezwa ni lazima juhudi za makusudi zichukuliwe ili jamii kuelimishwa na wao kushiriki katika kukabilina na tishio la Ebola hata kwa vijiji ambavyo vipo pembezoni.
Kama alivyosema Dk. Said, Mwenyekiti mwezeshaji kutoka wizara ya afya na ustawi wa jamii alisema anafurahishwa ushirika na wadau umepelekwa hadi katika radio za jamii ambazo ni muhimu sana katika kuimarisha juhudi za kufikia wananchi waliopo pembezoni.
005
Wamiliki wa Redio za Kijamii wakiwa katika mkutano ulioandaliwa na UNESCO, WHO, UNICEF, Wizara ya Afya na Ustawi ya Jamii ili kuwaelimsha wa wamiliki hao kutoa taarifa zilizo sahihi kwa wananchi kuhusu ugonjwa wa Ebola.

006

Tags: SIASAUCHUMI
ADVERTISEMENT
I am Magnifico

I am Magnifico

Related Posts

Wanafunzi Waliofadhiliwa Shule Binafsi Kuanza Kupewa Mkopo Vyuoni
BODI YA MIKOPO

Wanafunzi Waliofadhiliwa Shule Binafsi Kuanza Kupewa Mkopo Vyuoni

by I am Magnifico
Sep 23, 2019
0

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof....

Read more
Walimu 16 Wakamatwa Kwa Kuruhusu Mwanafunzi Feki Afanye Mtihani

Walimu 16 Wakamatwa Kwa Kuruhusu Mwanafunzi Feki Afanye Mtihani

Sep 13, 2019
Chuo Kikuu UDSM Chakanusha Matokeo Mabaya Kwa Wanafunzi Wake

Chuo Kikuu UDSM Chakanusha Matokeo Mabaya Kwa Wanafunzi Wake

Aug 29, 2019
SERIKALI YAWAPIGA MARUFUKU WALIMU KUINGIA DARASANI NA VIBOKO

SERIKALI YAWAPIGA MARUFUKU WALIMU KUINGIA DARASANI NA VIBOKO

Aug 1, 2019
VYUO VILIVYOKUWA VIMEFUNGIWA KUDAHILI VYAPEWA RUHUSA YA KUDAHILI

VYUO VILIVYOKUWA VIMEFUNGIWA KUDAHILI VYAPEWA RUHUSA YA KUDAHILI

Jul 16, 2019

SIKU YA MTOTO WA AFRIKA: Je adhabu ya kiboko shuleni iondolewe? Waziri azungumza

Jun 20, 2019
Next Post

DOWNLOAD NEW SONG | IZZO BIZNESS ( @Izzo_bizness ) FEAT G-NAKO ( @GnakoWarawara ) - HAINA KUFELI

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

I agree to the Terms & Conditions and Privacy Policy.

Currently Playing

KRANTZ MWANTEPELE (FOUNDER & CEO)

ADVERTISEMENT

KONCEPT TV

https://www.youtube.com/watch?v=0HP0mB_rtIU&t=7s
ADVERTISEMENT
Mwanaharakati Mzalendo

Mwanaharakati Mzalendo ni mtandao namba moja kwa habari makini kutoka pande zote za dunia kuhusiana na Michezo, Siasa, Afya, Elimu, Mahusiano, Vituko, n.k

Wasiliana nasi kwa Email;krantzcharles@gmail.com
SIMU; 0658123310

Follow Us

November 2014
M T W T F S S
« Oct   Dec »
 12
3456789
10111213141516
17181920212223
24252627282930
Currently Playing
  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

Login to your account below

Forgotten Password?

Fill the forms bellow to register

*By registering into our website, you agree to the Terms & Conditions and Privacy Policy.
All fields are required. Log In

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In