Serikali yakifunga kile chuo ‘feki’ cha Kilimo – Mwanaharakati Mzalendo
ADVERTISEMENT
  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Mwanaharakati Mzalendo
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
No Result
View All Result
Home ELIMU

Serikali yakifunga kile chuo ‘feki’ cha Kilimo

I am Magnifico by I am Magnifico
Nov 11, 2014
in ELIMU, KILIMO
0 0
0
0
SHARES
24
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter
ADVERTISEMENT

Kulia ni Richard Mchomvu mkuu wa Polisi wilaya ya Mbeya akiwa na jalada la uchunguzi kuhusiana na chuo hicho.
Serikal imekifunga Chuo cha Kilimo na Mifugo cha Nice Dream kilichopo mtaa wa Mapelele Kata ya Ilemi Jijini na kuwataka wanachuo wa chuo hicho kuondoka chuoni hapo baada ya siku tatu.

Agizo hilo lilitolewa na Kaimu Katibu Tawala Wilaya ya Mbeya Bi. Quip Mbeyela aliyemwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Daktari Norman Sigala na kwamba Serikali itagharamia chakula kwa siku tatu ambapo Serikali ilikabidhi shilingi laki tatu kwa Mtendaji Kata Bi Gladness Sapuka kwa ajili ya
kununua chakula kwa wanachuo 48 waliokuwa wakisoma katika chuo hicho ambacho hakina usajili kutoka Baraza la Vyuo (NACTE).

Imeelezwa kuwa, wamiliki wa chuo hicho walitumia kwa hadaa jina la Mhe. Frederick Sumaye, kuuaminisha umma kuwa Waziri Mkuu huyo mstaafu ndiye aliyezindua chuo hicho.
Mbali ya chuo hicho kutosajiliwa na NACTE, pia mmiliki wake hafahamiki vyema. Kaimu Katibu Tawala aliambatana na Mkuu wa Polisi Wilaya ya Mbeya Richard Mchumvu ambaye alisema kuwa Jeshi la Polisi linamtafuta mtuhumiwa na kwamba pindi atakapopatikana atafikishwa mahamani ili kujibu tuhuma za kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu kwa kutumia kivuli cha chuo na kuwatapeli wanachuo 48 waliokuwa na nia ya kusomea taaluma ya kilimo.


Kauli hiyo ilikuwa mwiba kwa wanachuo hao pale Kaimu Katibu Tawala aliposema kwamba Serikali haina chuo cha kuwapeleka kwa kuwa hakuna nafasi katka Vyuo vya Kilimo Mkoani Mbeya na muda wa usajili wa wanavyuo vya kilimo umemalizika.
Baadhi ya wanafunzi wakiwa hawaamini tamko lililotolewa na Selikari juu ya kufungwa chuo chao
  • Mbeya Yetu: SERIKALI YAKIFUNGA CHUO FEKI CHA KILIMO MBEYA
Tags: SERIKALI
ADVERTISEMENT
I am Magnifico

I am Magnifico

Related Posts

Wanafunzi Waliofadhiliwa Shule Binafsi Kuanza Kupewa Mkopo Vyuoni
BODI YA MIKOPO

Wanafunzi Waliofadhiliwa Shule Binafsi Kuanza Kupewa Mkopo Vyuoni

by I am Magnifico
Sep 23, 2019
0

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof....

Read more
Walimu 16 Wakamatwa Kwa Kuruhusu Mwanafunzi Feki Afanye Mtihani

Walimu 16 Wakamatwa Kwa Kuruhusu Mwanafunzi Feki Afanye Mtihani

Sep 13, 2019
Chuo Kikuu UDSM Chakanusha Matokeo Mabaya Kwa Wanafunzi Wake

Chuo Kikuu UDSM Chakanusha Matokeo Mabaya Kwa Wanafunzi Wake

Aug 29, 2019
SERIKALI YAWAPIGA MARUFUKU WALIMU KUINGIA DARASANI NA VIBOKO

SERIKALI YAWAPIGA MARUFUKU WALIMU KUINGIA DARASANI NA VIBOKO

Aug 1, 2019
WAKULIMA WA PAMBA KUPEWA VITAMBULISHO

WAKULIMA WA PAMBA KUPEWA VITAMBULISHO

Jul 19, 2019
VYUO VILIVYOKUWA VIMEFUNGIWA KUDAHILI VYAPEWA RUHUSA YA KUDAHILI

VYUO VILIVYOKUWA VIMEFUNGIWA KUDAHILI VYAPEWA RUHUSA YA KUDAHILI

Jul 16, 2019
Next Post

Baada ya Mbatia (NCCR-Mageuzi) Makyao (CHADEMA) atangaza kuwania Vunjo ya Mrema (TLP)

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

I agree to the Terms & Conditions and Privacy Policy.

Currently Playing

KRANTZ MWANTEPELE (FOUNDER & CEO)

ADVERTISEMENT

KONCEPT TV

https://www.youtube.com/watch?v=0HP0mB_rtIU&t=7s
ADVERTISEMENT
Mwanaharakati Mzalendo

Mwanaharakati Mzalendo ni mtandao namba moja kwa habari makini kutoka pande zote za dunia kuhusiana na Michezo, Siasa, Afya, Elimu, Mahusiano, Vituko, n.k

Wasiliana nasi kwa Email;krantzcharles@gmail.com
SIMU; 0658123310

Follow Us

November 2014
M T W T F S S
« Oct   Dec »
 12
3456789
10111213141516
17181920212223
24252627282930
Currently Playing
  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

Login to your account below

Forgotten Password?

Fill the forms bellow to register

*By registering into our website, you agree to the Terms & Conditions and Privacy Policy.
All fields are required. Log In

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In