Mwanaharakati Mzalendo

HUKUWA UNAFAHAMU HILI KUHUSU MWANADADA TARAJI P. HENSON

Taraji P. Henson alizaliwa September 11,1970 na ni mwigizaji mashuhuri huko Hollywood aliyejizolea mashabiki kote Ulimwenguni akitamba kupitia filamu na maigizo ya runinga maarufu alizocheza kama vile Person of Interest aliyoigiza kama Detective Jocelyn Carter, Filamu ya Think Like a Man na Think Like a Man Too pamoja na Igizo la Runingani linalotamba kwa sasa linalojulikana kama Empire aliyoigiza kama Cookie Lyon, mke wa bilionea Lyon ambao kwa pamoja walitoka katika umasikini mkubwa na kubadilisha kidogo walichokuwa nacho na kuunda kampuni kubwa kabisa inayojihusisha na maswala ya muziki.
USILOLIFAHAMU KUHUSU TARAJI P. HENSON
Taraji alizaliwa kwa wazazi Boris Lawrence Henson na Bernice Gordon, na walimpa jina la TARAJI PENDA ikiwa ni jina lenye asili ya Lugha izungumzwayo Afrika Mashariki, Lugha ya Kiswahili, ikiwa na maana ya HOPE/EXPECT LOVE.
Taraji anasifika kwa uamuzi wake mgumu wa kuacha kazi aliyoisomea Chuo Kikuu huku akiwa na dola 700 tu mfukoni, na kuamua kuanza kutimiza ndoto zake za kuwa muigizaji, na kwa Hakika ni dhahiri amefanikiwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *