Mwanaharakati Mzalendo

Kanye West apamba jarida la PAPER.

american_dream_kanye_west_april_cover.jpg
“Najua watu wanaota juu ya Marekani lakini mimi naota juu ya Dunia” – Kanye West.
Ikiwa ni miezi kama sita hivi imepita tangu mama watoto wa Kanye West, Kim Kardashian alipambe jarida la PAPER sasa imekuwa ni zamu ya staa huyo mwenye vipaji lukuki kulimeremetesha jarida hilo huku akilighubika kwa siri zake nyingi za kimaisha. November 2014 Kim Kardashian alibaki mtupu kulipamba jarida hilo na April 2015 baba wa North West amejaa yeye kwenye PAPER. 

kanyewest_spread_1.jpg

Kanye ambaye ni Muandaaji wa Muziki (Produza), Rapa na Mbunifu wa Mavazi (Mwanamitindo) ameongea mengi sana kunako jarida hilo lakini zaidi amegusia mapito yake katika maisha ya kawaida na maisha ya sanaa.
Kanye amezungumzia ubaguzi aliowahi kufanyiwa nchini China kwani amesema kuwa akiwa na umri wa miaka 10 aliishi China na wakati huo watoto wa kichina walikuwa wakimsugua usoni kuona kama ngozi yake nyeusi itatoka. Akielezea ubaguzi kwa undani Kanye amesema ni suala zito sana ambalo pia linabadilika kulingana na wakati kwani kipindi anakua na kipindi hiki ambacho teknolojia imetengemaa mtazamo wa ubaguzi unabadilika.

kanye_spead_3.jpg

Kuhusu sanaa Kanye amegusia jinsi alivyotokea kupenda kuwa Mbunifu wa Mavazi, Kanye amesema wakati yuko High School akiwa na miaka 15 alifanya kibarua katika kampuni ya Gap na hapo ndipo alianza kuvutiwa na mavazi na kuanza kufikiri kufanya mambo ambayo anayafanya sasa. Rapa huyo amesema mbali na vipaji vingine yeye pia ni Mchoraji, lakini hakusita kubainisha kuwa mapenzi yake amewekeza kwenye Mitindo na wala sio muziki.
Akiteta kuhusu maisha ya kawaida, Kanye ameeleza kuwa akimtazama mwanaye North huwa anaweza kuona uhalisia wa maisha, mbali na maisha ya sanaa ambayo anaishi kwa muda mrefu.
Picha: PAPER MAGAZINE.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *