Mwanaharakati Mzalendo

Wema aibua mazito na kuwabwatukia Nuhu na shilole


wemasepetu.jpgWema Sepetu

LILE sakata la mrembo Wema Sepetu kutakwa kimapenzi na mpenzi wa msanii mwenzake, Zuwena Mohamed ‘Shilole’, Nuh Mziwanda limeendelea kushika kasi ambapo Wema ameibuka na kuwavua nguo kwa kuwatolea maneno ya shombo.
nuhumziwanda.pngNuh Mziwanda na Shilole.
Wema alitoa maneno hayo hivi karibuni baada ya Shilole na Nuh kumgeuka na kusema kwamba aliwachezea mchezo mchafu ili kuwagombanisha kwa sababu anawaona wanapendana hivyo alimtafuta mtu ambaye anaendana na sauti ya Nuh ili tu amharibie.

“Sijui kwa nini Wema kanifanyia hivi najua anataka tu kunigombanisha na mpenzi wangu kwa sababu hata ukisikiliza hiyo rekodi utasikia sauti ya Mirror akizungumza, hapo ndiyo ujue kuna mchezo mchafu sana na kwa hilo amefanikiwa lakini sisi huku mapenzi yetu yanaendelea,” alisema Nuhu.

Kutokana na maneno hayo Wema alicharuka na kusema kwamba hawezi kutoa rekodi ya uongo na kumsingizia Nuh kwani ni mpuuzi na hawezi kujilinganisha naye kutokana na kwamba ni staa mkubwa.

“Nuh alinipigia na kunitaka kimapenzi ndipo nikaamua kumrekodi na hiyo ni sauti yake haijatengenezwa kama wao wanavyodai, kwanza nawashangaa hivi ningetengeneza sauti feki ili iweje, Nuh na Shilole siyo levo yangu ni wasanii wachanga sana, mimi ni staa mkubwa Tanzania na hakuna wa kulinganishwa na mimi labda nje ya Bongo. Nitafute kiki kwa kina Shilole  na Nuh kweli? Si bora nitengeneze kiki kwa kina Davido na wasanii wengine wakubwa duniani, hao si levo yangu jamani,” alisema Wema kwa sauti ya hasira.

Kabla ya kupatana, Nuh na Shilole waligombana hivi karibuni katika Viwanja vya Leaders Club, Kinondoni baada ya mrembo huyo kupokea sauti hiyo iliyosikika Nuh akimtongoza Wema.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *