Mwanaharakati Mzalendo

Diamond Platnumz Kurudi Bongo leo Tuzo 5 , Ipo HapaHabari ya Diamond kushinda tuzo 3 kwenye AFRIMMA nchini marekani imekuwa gumzo sana pia kukutana na watu wa Nafca “Nollywood & African Film Critics’ Awards” pia wakamkabidhi tuzo zake 2 alizowahi kushinda siku za nyuma imezidi kumpaisha zaidi na kumfanya awe na tuzo 5 ambazo yupo nazo marekani na atazileta bongo kesho kwa mashabiki wake na watu wa nyumbani.Diamond Platnumz Amepost Picha Hio Hapo Juu huku akiweka maneno haya “Inshaallah Panapo Majaaliwa alhamisi hii saa saba na dakika 25 Mchana Mwanenu natua na tuzo zote mloniagiza toka Nchini Marekani… Niko naongea na Uongozi wa Escape One ili ikiwezekana kutokea Airport kwa pamoja tuelekee direct pale Ecape One ili wote tuweze Piga picha na Tunzo hizi na Kuburudika kwa Kiingilio cha BURE!!!! kabisa Hadi tuchoke…. Tunzo Hizi ni zetu sote, Hivyo tueke Itikadi ya Vyama na Tofauti ya aina yoyote pembeni na kwa Pamoja tutangulize UTAIFA MBELE….. nimefrai sana kupokea habari kuwa ndugu zetu toka nchi za karibu kama Kenya, Uganda, Rwanda , Burundi Congo Etc…. pia watakuja kufurahi nasi pamoja….. HIZI NI TUNZO ZA WANAMASHARIKI na AFRICA kwa Ujumla.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *