Mwanaharakati Mzalendo

Mbasha Afunguka Mazito, Asema Hawezi Kumsahau FloraSiku chache baada ya mwimbaji wa nyimbo za Injili, Flora Mbasha kufuta kesi ya kudai talaka mahakamani na kudai kuwa bado ana ‘mapenzi’ na mumewe, Emmanuel Mbasha ameibuka na kujiapiza kuwa kutokana na ukali wa mateso aliyoyapitia wakati wa kesi yake, kamwe hawezi kumsamehe mwanamke huyo.
Aliyekuwa mke wa Emmanuel Mbasha, Flora Mbasha.

Akizungumza na Ijumaa kwa njia ya simu, Jumatano ya wiki hii siku moja baada ya Flora kuamua kufuta kesi hiyo katika Mahakama ya Kisutu jijini Dar, Mbasha alilalamikia yale aliyofanyiwa na mwenza wake huyo kipindi cha nyuma kiasi cha kutoona sababu ya kurudiana naye.

MSIKILIZE KIDOGO MBASHA
“Flora ni mwanamke muongo na mnyama, anawezaje kujitokeza hadharani kipindi hiki na kudai kuwa amefuta kesi ya talaka na kwamba ananipenda, kweli? Ni wiki mbili tu zilizopita nilikuwa hatarini kwenda jela kwa zaidi ya miaka 30, alikuwa wapi kuja kunitetea na kufuta kesi hiyo? Alikuwa wapi huyu?

“Kaniharibia kila kitu, maisha yangu yaliyumba kwa kuwazia kesi ya kusingiziwa kubaka, kama siku ya kesi pale mahakama ya Ilala ningefungwa, leo hii angeyasema hayo?

HATAKI HATA KUMUONA!
Katika hali isiyokuwa ya kawaida, licha ya kuwa ni mzazi mwenzake, Mbasha alisema hataki hata kumuona Flora kwa kile alichokiita “kukaa mbali na wakala wa shetani” na kwamba kamwe hawezi kumsamehe.

“Kaka, afanye maisha yake, sitaki hata kumona na kamwe siwezi kumsamehe Flora kabisa, never (kamwe),” alisema Mbasha.

TUJIKUMBUSHE NYUMA
Mnamo Septemba 21, mwaka huu Mbasha aliachiwa huru dhidi ya madai ya kesi iliyokuwa ikimkabili ya kumbaka shemeji yake, katika Mahakama ya Ilala, jijini Dar ambapo Jumanne ya wiki hii alifikishwa tena katika Mahakama ya Kisutu jijini Dar na Flora akimdai talaka.
Source: GPL

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *