Mwanaharakati Mzalendo

Mghwira Akubali Yaishe, Ampongeza Magufuli

Mgombea wa ACT – Wazalendo, Anna Mghwira.

Mgombea wa ACT – Wazalendo, Anna Mghwira.

Mgombea wa chama cha  ACT – Wazalendo, Anna Mghwira amekubali ushindi wa mgombea wa CCM Dkt John Pombe Magufuli katika uchaguzi mkuu uliohitimishwa  jana katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es salaam.

Kufuatia Magufuli kutangazwa mshindi  Mghwira  alimpigia simu Dk Magufuli muda mfupi baadae na kumpongeza.
Kwa upande wake  Dk Magufuli alimshukuru mgombea huyo wa upinzani na kumwita mkomavu wa siasa na mwanademokrasia wa mfano wa kuigwa nchini Tanzania.
Katika uchaguzi huo, ambao wagombea wa urais walikuwa wanane, mwanamke pekee, Anna Mgwhira wa chama kipya cha ACT-Wazalendo alishika nafasi ya tatu kwa kupata kura 98,763 sawa na asilimia 0.65.
Aidha, Dk Magufuli alitangazwa mshindi  alifuatiwa na mgombea wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) aliyeungwa mkono na vyama vinne vya upinzani (Ukawa), Edward Lowassa aliyepata kura 6,072,848, sawa na asilimia 39.97 ya kura halali zilizopigwa.
Wagombea wengine kura walizopata na asilimia kwenye zake  ni Chief Lutalosa Yemba wa ADC kura 66,049 (asilimia 0.43), Hashim Rungwe wa Chaumma kura 49,256 (asilimia 0.32), Janken Kasambala wa NRA kura 8,028 (asilimia 0.05), Macmillan Lyimo wa TLP kura 8,198 (asilimia 0.05), Fahmi Dovutwa wa UPDP kura 7,785 (0.05%)
.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *