Mwanaharakati Mzalendo

MAKALA;MAFANIKIO YA MUZIKI WA DAVIDO SASA SHAKANINa Kennedy Mmari 

Wakati soko la muziki
wa Kiafrika likiendelea kukua na kuimarika kwa kasi huku vipaji vipya
vikiendelea kuchomoza kutoka kila pande ya Afrika, soko la muziki kwa Star wa
Nigeria Davido Adeleke almaarufu Davido linaonekana kupungua na kuzidiwa kwa
kasi na mastaa wengine, Mwanaharakati Mzalendo inaweza kuthibitisha.

Davido, ambaye
amejizolea umaarufu mkubwa ulioambatana na tuzo kedekede katika katika kipindi
cha miaka mitatu iliyopita amekuwa akiendelea kupata view chache katika video
zake za YouTube katika kila video mpya ambayo anaendelea kutoa.

Katika Video zake alizotoa
hivi karibuni ambazo wengi walitarajia zingekuwa na mafanikio makubwa kama vile
Fans Mi Ft Meek Mill ina views milioni 3 ndani ya miezi mitano, Video ya Dodo
yenye mwezi mmoja ina views laki 8 wakati video ya hivi karibuni ya The Money
yenye wiki moja ikiwa na views laki mbili na elfu sitini na nne kufikia tarehe
15 November 2015.

Kiashiria hiki cha
kushuka kwa mapenzi ya mashabiki kwa muziki wa Davido kinakuja huku wasanii
wengine wakubwa kama Diamond Platnumz wakiendelea kufurahia kukua na kuongezeka
kwa watazamaji katika video zao za YouTube.
Wakati video ya Fans Mi
ikiwa na watazamaji milioni 3, Video ya Nana ambayo zilitoka wakati mmoja ina
watazamaji milioni 6.

Wakati video ya The
Money ikiwa na siku 9 na watazamaji laki mbili unusu, Video ya Nana ya Diamond
ndani ya siku 10 ilikuwa na watazamaji milioni 1.

Nini maoni yako? Hili
ni anguko la Davido kama moja kati ya wasanii vinara barani Afrika?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *