Mwanaharakati Mzalendo

Mourinho: Nitawapumzisha Wachezaji Dhidi ya Arsenal

Jose Mourinho amesema kuwa atawapumzisha wachezaji walioshiriki mechi nyingi dhidi ya Arsenal


Mkufunzi wa klabu ya Manchester United Jose Mourinho anasema kuwa atawapumzisha wachezaji wake katika mechi ya siku ya Jumapili dhidi ya Arsenal.

Ushindi mwembamba wa 1-0 dhidi ya klabu ya Uhispania Celta Vigo siku ya Alhamisi ulikuwa wa 10 tangu mwezi Aprili.

Huku kikosi hicho cha Mourinho kikiwa katika nafasi ya tano katika jedwali la ligi ya Uingereza, ligi ya kombe la Europa inaweza kuwapatia fursa ya kushiriki katika kombe la vilabu bingwa Ulaya msimu ujao.

”Wachezaji ambao wameshiriki katika mechi nyingi hatawachezeshwa wikendi”, alisema Mourinho.

Mpira wa dhabu wa Marcus Rashford uliipatia United ushindi katika awamu ya kwanza ya mechi ya marudio nchini Uhispania huku awamu ya pili ikitarajiwa Alhamisi ijayo katika uwanja wa Old Trafford.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *