Harmonize Ataja Sababu Zakutemana na Mpenzi Wake

Msanii kutokea WCB, Harmonize amewekaza wazi kile kilichotokea kati yake na mpenzi wake, Sarah.


Wiki iliyopita  Harmonize aliweka wazi kwa sasa yupo single na maswali kuibuka iwapo amemwagana na bibie.

Sasa muimbaji huyo amesema kilichotokea alikuwa na show nchini Ghana na mpenzi wake alikuwa akimpigia simu na kumkosa ndipo akapeleka suala hilo katika mitandao kitu ambacho hakupendezwa nacho.

“Unapoamua kuwa na mtu unatakiwa ujue huyo mtu ni wa aina gani, anafanya kazi gani, ukishajua hivyo unakuwa ni rahisi zaidi ku-deal naye,” amesema.

“Nakutana na watangazaji, wasanii inatakiwa ni badilishane nao mawazo, sasa ukiwa unaendekeza kila saa masuala ya kimahusiano inakuwa unanirudisha nyuma kwa namna moja au nyingine,” Harmonize ameiambia Wasafi TV.

Harmonize ameongeza kuwa kwa namna moja au nyingine mpenzi wake, Sarah ameshindwa kuolewa yeye ni mtu wa namna gani kwani anapokutana na wasanii wengine au watangazaji wa nje na kupiga nao picha tayari ni ugomvi wakati yeye anatakiwa kufanya hivyo ili kuusogeza muziki wake mbele.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *