Mwanaharakati Mzalendo

KUBENEA AMBANA WAZIRI KABUDI KUHUSIANA NA FEDHA ZA MAKINIKIA

Mbunge wa Ubungo (Chadema), Saed Kubenea
amemtaka Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Palamagamba Kabudi kulieleza Bunge
majadiliano baina ya Serikali na Kampuni ya Madini ya Acacia kuhusu makinikia
yamefikia wapi.

Akichangia hotuba ya Bajeti ya wizara ya
Madini Bungeni mjini Dodoma, Kubenea amemtaka Waziri Kabudi kutoa taarifa
kuhusiana na Dola Bilioni 190 ambazo ni zaidi ya Sh 424 trilioni zinazopaswa
kulipwa na Acacia zitapatikanani lini.

Kubenea amesema fedha hizo Sh424 trilioni
zinapaswa kila Mtanzania apate matibabu, kuishi maisha mazuri kwa fedha hizo
zinapatijkana lini?

Na Amos C Nyanduku

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *