Mwanaharakati Mzalendo

NEC yatangaza tarehe ya Uchaguzi mdogo Jimbo Moja na Kata 79

Tume ya Taifa ya Uchaguzi  (NEC) itafanya uchaguzi mdogo kwenye Jimbo la Buyungu, Mkoani Kigoma na kwenye Kata 79 za Tanzania Bara, Mwenyekiti wa NEC, Jaji (R), Semistocles Kaijage amesema.
Akizungumza Jijini Dar es Salaam, Jaji Kaijage amesema uchaguzi huo utafanyika tarehe 12 mwenzi Agosti na fomu za uteuzi wa wagombea zitatolewa kuanzia tarehe 8 hadi 14 Julai.

“Uteuzi wa Wagombea utafanyika tarehe 14 Julai, mwaka huu. Kampeni za Uchaguzi zitafanyika kati ya tarehe 15 Julai, hadi tarehe 11 Agosti, mwaka huu na siku ya uchaguzi itakuwa ni tarehe 12 Agosti mwaka huu,” amesema Jaji Kaijage.

Jaji Kaijage amebainisha kwamba Tume imetangaza uwepo wa nafasi wazi ya Ubunge kwenye Jimbo hilo la Buyungu baadaya kupokea taarifa kutoka kwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano, Ndugu Job Ndugai baadaya ya kifo cha aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo.

Kwa upande wa nafasi wazi za Udiwani, Jaji Kaijage amesema Tume ilipokea taarifa kutoka kwa Waziri wa Tamisemi akiitaarifu juu ya uwepo wa nafasi hizo na taratibu za uchaguzi mdogo zikaanza mara moja.

Jaji Kaijage amesema kuwa uchaguzi huo mdogo utafanyika ndani ya Halmashauri 43 zilizopo kwenye Mikoa 24 ya Tanzania Bara, na Mikoa hiyo ni pamoja na, Kigoma, Arusha, Dar es Salaam, Dodoma, Iringa, Kagera, Katavi, Kilimanjaro, Lindi, Manyara, Mara, Mbeya, Mtwara, Morogoro, Mwanza, Njombe, Rukwa, Ruvuma, Shinyanga, Simiyu, Singida, Songwe, Tabora naTanga. 

==

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *