Mwanaharakati Mzalendo

MKUU WA WILAYA YA CHUNYA AAHIDI KUPAMBANA NA WAFUGAJI WANAOHALIBU VYANZO VYA MAJI

Mkuu
wa Wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya  Meryprisca Mahundi (katikati)
akimkisikiliza kwa makini Afisa Mtendaji Kata ya Sangambi kijiji cha
Igundu  Joseph Nangale ,kuhusiana na namna ambavyo wafugaji wamefanya
uhalibifu wa vyanzo vya maji katika kjiji hicho.Picha David Nyembe
Mkuu
wa Wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya  Meryprisca Mahundi akiwa katika
harakati za kujionea maeneo ya vyanzo vya maji  ambayo yamehalibiwa
vibaya na baadhi ya wafugaji wa kijiji cha Igundu kutokana na kunywesha
mifugo katika maeneo hayo .
Mkuu
wa Wilaya ya Chunya Mh Meryprisca Mahundi (Katikati)akiteta jambo na
viongozi wa vijiji vinavyo zunguka kata ya Sangambi ambako kumefanyika
uhalibifu wa vyanzo vya maji kutokana na baadhi ya wafugaji wa vijiji
hivyo kunywesha mifugo yao sanjali na kupitisha mifugo katika maeneo ya
vyazno hivyo.
Mkuu
wa Wilaya ya Chunya Mh Meryprisca Mahundi akizungumza na wananchi wa
Kata ya Sangambi (hawapo pichani) mara baada ya kukamilisha ziara ya
kutembelea maeneo ya vyanzo vya maji  ambako kumefanyika uhalibifu
mkubwa kutokana na baadhi ya wafugaji kupitisha mifugo yao  .
Wananchi
wa kijiji cha Igundu  wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Chunya
Merryprisca Mahundi (hayupo pichani) mara baada ya kukamilisha ziara ya
kutembelea maeneo ya vyanzo vya maji  ambako kumefanyika uhalibifu
mkubwa kutokana na baadhi ya wafugaji kupitisha mifugo yao  .Na David Nyembe, Chunya


MKUU wa Wilaya ya Chunya mkoani Mbeya, Maryprisca Mahundi,
amewapa wiki tatu wafugaji wa Kijiji cha Igundu katika Kata ya Sangambi
wilayani humo kuhamisha mifugo yao na kuipeleka katika Kijiji cha Paris ambacho
kimetengwa kwa ajili ya wafugaji.


Ametoa kauli hiyo   wakati wa Mkutano wa Hadhara uliofanyika
kijijini hapo ambapo alisema lengo la kuondoa mifugo hiyo ni kumaliza mgogoro
kati ya wakulima wa kijiji hicho na wafugaji pamoja na kuokoa chanzo cha maji
ambacho wakazi wa eneo hilo wanakitegemea.


Alimuagiza Ofisa Mtendaji wa Kijiji hicho, Joseph Nangale,
kusimamia na kuhakikisha mifugo hiyo inahamishwa huku akimtaka kutumia nguvu
iliyotumika kuwazuia wakulima kufanya shughuli zao karibu na chanzo cha maji.


Mahundi alisema amechoshwa na migogoro ya wakulima na
wafugaji katika kijji hicho cha Igundu na kwamba agizo lake hilo ni la mwisho
na kwamba atakaporudi tena kwenye kijiji hicho na kukuta inaendelea hakutakuwa
na majadiliano tena na kwamba wasije wakamlaumu.


“Mkae chini mjadiliane na mkubaliane idadi ya mifugo ambayo
kila mfugaji wa kijiji hiki atatakiwa kubaki nayo hapa, nimewapa siku 10
viongozi wenu waniletee taarifa ya majidiriano hayo, lakini nimewashauri kila
mfugaji abaki na mifugo 10,” alisema Mahundi.


Alisema idadi hiyo aliyopendekeza kila mfugaji abaki nayo
kijijini hapo ni rahisi kuimudu ili isiingie kwenye mazao ya wakulima na kwamba
itasaidia kumaliza migogoro.


Ofisa Mtendaji wa Kijiji hicho, Nangale alikiri kijiji hocho
kuwa na idadi kubwa ya mifugo kuliko uwezo wa eneo la kijiji hicho hali ambayo
inapelekea migogoro ya mara kwa mara kati ya wakulima na wafugaji.


Alisema migogoro hiyo ilikuwa inaibuka baada ya mifugo
kuwashinda wafugaji na kuingia kwenye mashamba ya wakulima na kuharibu mazao na
hivyo kuwafanya wakulima waanze kutaka kulipiza kisasi.


Aliahidi kushiriiana na halmashauri nzima ya kijiji hicho
katika kutekeleza agizo la Mkuu wa Wilaya la kuondoa mifugo na kwamba
watayashirikisha makundi yote ili kufikia mwafaka ambao hautaleta shida.


“Kijiji cha paris kina eneo kubwa kwa ajili ya mifugo na ni
eneo rafiki kwa sababu hakuna mwingiliano na shughuli zingine za kibinadamu,
tulikitenga maalumu kwa ajili ya wafugaji,” alisema Nangale.


Katika hatua nyingine Mkuu wa Wilaya aliwatahadharisha
viongozi wa vijiji wanaopokea rushwa kutoka kwa wafugaji ili waingize mifugo
kwenye vijiji vyao kuwa watachukuliwa hatua kali za kisheria endapo
watabainika.


.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *