Mwanaharakati Mzalendo

Baada ya sakata lake la unyanyasaji mabinti kingono kupoa, R Kelly atangaza Tour katika mataifa haya barani Ulaya


Baada ya sakata lake la unyanyasaji mabinti kingono kupoa, R Kelly atangaza Tour katika mataifa haya barani Ulaya

Ikiw alipitia wakati mgumu sana katika majuma kadhaa nyuma kuhusiana na unyanyasaji wa kingono, Nguli wa R&B duniani R. Kelly ameamua kutangaza balaa barani Ulaya akitarajia kuatafanya tour katika nchi tofauti barani Ulaya.


Jana aliamua kuchukua jukumu hilo kupitia mitandao ya kijamii na kueleza mpango wake wa tour ya muziki katika nchi ya Australia, New Zealand, na Sri Lanka, pia amepanga kufanya show nchini Ujerumani mwezi Aprili.


Mipango hiyo imekuja baada ya mwimbaji huyo kukataa mashtaka yanayomkabili dhidi yake na kwamba hakuwa na hatia ya uhalifu wowote wa ngono, licha ya documentary “Surviving R. Kelly” iliyodondoka mtaani ikionyesha namna jamaa alivyokuwa anafanya unyanyasaji wa kijinsia, kimwili na kiakili kwa wasichana wenye umri wa chini ya 18.


“Kutokana na hali ya sasa katika maisha ya R Kelly binafsi na ugomvi unaozunguka naye, wahamasishaji wameamua kusonga mbele na wanazingatia matukio mengine,” walisema. Ziara hiyo mpya ilitangazwa kupitia kurasa za Twitter, Facebook na Instagram. ingawa promotor Flamingo Dreamz, hakujibu ombi la Guardian la kutoa maoni.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *