Mwanaharakati Mzalendo

Channel Ten na Magic Fm mikononi mwa CCM, Rais Magufuli aeleza


Channel Ten na Magic Fm mikononi mwa CCM, Rais Magufuli aeleza

Rais Dkt. John Pombe Magufuli amesema Africa Media Group (Channel Ten na Magic Fm) ni mali ya Chama Cha Mapinduzi.

Amesema hayo leo alipotembelea Kituo hicho ambapo ameahidi kukabidhi Mil 100 ifikapo kesho kwa ajili ya ununuzi wa vifaa vikiwemo Camera.

“Chama chetu cha mapinduzi kwa sababu kinatimiza miaka 42 tangu kianzishwe, kwa hiyo nilifikiri ngoja niende Africa Media Group niwasalimu kwa sababu ni chombo cha Chama cha Mapinduzi,” amesema Rais Magufuli.

Rais Magufuli aliendelea kwa kusema, ‘Kwanza nataka kuwadhibitishia mimi huwa napenda kuangalia Channel Ten, kwa hiyo mimi ni shabiki wenu,’.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *