Mwanaharakati Mzalendo

Coca Cola YAZINDUA KAMPENI YA MCHANGA PEKEE LEO JIJINI DAR ES SALAAM

Mkurungenzi Mkuu wa Coca Cola Kwanza anaitwa Basil Gadzios Akiongea na mamia ya wakazi wa dar waliojitokeza katika kuunga mkono kampeni ya Mchanga Pekee.

 Leodegar Tenga, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirikisho la Viwanda Tanzania akitoa pongezi kwa Coca Cola Tanzania

Wafanyakazi wa Coca Cola Kwanza na Wananchi wengine waliojitokeza wakifanya mazoezi ya kuchangamsha mwili (Aerobics) mapema asubuhi.

Msanii na Balozi wa Coca Cola Kwanza Mrisho Mpoto (Mjomba) akitoa burudani na ujumbe kwa jamii iliyokusanyika hapa.


 Mkurungezi mtendaji wa EcoAct TanzaniaChristian Mwijage akielezea jinsi wanavyotumia Chupa za Plastic kutengenezea bidhaa mbalimbali, ikiwemo vibao vya tahadhari vya barabarani.

Bw. Geofrey Tengeneza, Afisa Uhusiano Mkuu wa TTB akiongea na wananchi kuhusu umuhimu wa kutunza mazingira ya bahari.

Mkurugenzi wa Taasisi ya Nipe Fagio.  Tania Hamilton,  akishiriki kusafisha fukwe ya Coco Beach

Mrisho Mpoto (kushoto) Basil Gadcious, Mkurugenzi mkuu wa Coca Cola Tanzania (Kati) na Tania Hamilton (Kulia) wakijadilia jambo.


MAUDHUI YA KAMPENI
YA
MCHANGA PEKEE
Mchanga Pekee
Mchanga pekee ni Kampeni iliobuniwa, kuasisiwa na kusimamiwa na Kampuni ya Coca-Cola kwanza Kampuni Tanzu ya Coca-Cola Beverages Africa yenye malengo na madhumuni ya kuelimisha, kufundisha na kuhimiza uhifadhi wa mazingira ya jamii zetu ikiwa imejikita katika ukusanyaji wa plastiki na usafishaji wa fukwe zetu.
Chimbuko la kampeni (Mchanga Pekee)
Shirika la International Council of Beverages Associations (ICBA) mwishoni mwa mwaka 2018 lilitoa ripoti inaoonyesha uchafuzi wa fukwe umefikia wastani wa vipande vya plastiki 13,000 kwa km2 za fukwe za baharini na utafiti wa karibuni umebaini kuwa kuna Tani million 150 za plastiki kwenye fukwe zetu duniani mpaka leo. Kupitia tafiti hizi na nyingine zilizopo Kampuni ya Coca-Cola kwanza imeamua kuja na Kampeni yenye malengo ya kuikumbusha na kuishirikisha jamii juu ya Utunzaji wa mazingira kwa ukusanyaji wa taka (plastiki), uhifadhi wake na Ubadilishaji wa matumizi wa plastiki (recycling) kwa manufaa bora ya jamii na mazingira kwa ujumla.
Mchanga Pekee ni nini?
Ni kampeni ya mazingira yenye malengo ya usafishaji wa fukwe zetu na kuziweka katika mandhari salama,endelevu na zenya kuvutia yaani kuubakiza mchanga peke yake kwenye fukwe kwa kuondoa vitu visivyostahili kuwepo (uchafu-plastiki) na pia kampeni itajikita katika ukusanyaji wa chupa za plastiki katika mazingira yetu kuwezesha mazingira kuwa salama na yenye kuweza kuhifadhi ekolojia ya mazingira iliopo.


Usafishaji fukwe.
Kama lengo moja wapo wa kampeni ya Mchanga pekee kampuni ya Coca-Cola Kwanza imefikia makubaliano na serikali (upande wa halmashauri) ya kufanya usafi wa fukwe, na fukwe ya Coco (coco beach) kama eneo la kuanzia kampeni yetu huku kampeni hii ikiwa na lengo la kufikia fukwe zote zilizopo nchini.
Coca Cola Kwanza itaajiri na kuwawezesha wanawake na vijana kwa kuwapa vitendea kazi na posho ya kufanya usafishaji wa fukwe kwa kipindi chote (mwaka mzima) ambapo watakuwa na jukumu la msingi la kuhakikisha fukwe inakuwa katika hali ya usafi muda wote na kuhamasisha utalii wa fukwe kwa kuwezesha wale wanao tembelea fukwe kufurahia mandhari ya fukwe hizo katika mazingira yalio safi na salama.


Ukusanyaji taka (chupa za Plastiki) 10,000/Mwezi
Kama sehemu ya Kampeni hii ya Mchanga pekee Coca-Cola Kwanza pia imejikita kukusanya Chupa za plastiki 10,000 kwa kila mwezi kwa lengo la kuelimisha jamii umuhimu wa ukusanyaji wa taka hizo (plastiki) na katika kampeni hii Coca-Cola Kwanza itazinunua chupa kutoka kwa jamii kupitia safari za utembeleaji wa jamii kwenye maeneo yao. Jamii itakusanya chupa na kampuni kuzinunua kwa bei iliopangwa kwa kipindi hicho, kampeni hii itaenda kwa kibwagizo chenye msemo wa “Trash 4 Cash”.
Faida na umuhimu wa Kampeni (Mchanga Pekee)
  1. Ufahamu na uelimishaji wa Uhifadhi na utunzaji endelevu wa mazingira yetu kwa ujumla.
  2. Kuunga mkono juhudi za serikali katika kujenga jamii bora yenye kutambua umuhimu wa uhifadhi wa mzingingira na usimamizi endelevu wa mazingira.
  3. Ukuzaji wa sekta ya utalii wa fukwe kwa kuwezesha utunzaji wa fukwe wa muda wote na kufanikisha mvuto wa fukwe kama sehemu moja wapo ya kipato cha taifa kupitia sekta ya utalii.
  4. Uwezeshaji wa kiuchumu na kifursa (ajira) kwa vijana na wanawake kupitia mradi huu (mchanga pekee)
  5. Kupunguza ongezeko la chupa za plastiki katika jamii na kufundisha jamii njia bora za uhifadhi na ubadilishi bora wa matumizi ya chupa za plastiki.
  6. Ulinzi na uhifadhi wa ekolojia ya viumbe vya baharini na nchi kavu pia kuwezehsa jamii kuishi kwenye maeneo yaliyo huru na uchafu na maradhi yatokanayo na uchafuzi wa mazingira.


Hitimisho
Kampuni ya Coca-Cola kwanza kama sehemu ya jamii na mdau mkubwa wa serikali na jamii katika uhifadhi wa mazingira imejipanga kuendeleza kampeni hii na kubuni kampeni nyingine tofauti tofauti zenye lengo la kuiwezesha jamii kuishi kwenye jamii ilio salama na endelevu ilikuwezesha shuguli za maendeleo kufanyika kwenye mazingira yalio bora na salama.
Imeandaliwa na
Idara ya mahusiano ya umma na mawasiliano
Coca-Cola kwanza


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *