Mwanaharakati Mzalendo

MAKAMU WA RAIS AWASILI IGUNGA MKOANI TABORA KUTEMBELEA MIRADI MBALIMBALI

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Tabora Mzee Hassan Wakasubi mara baada ya kuwasili Igunga, katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Aggrey Mwanri. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Mheshimiwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo ameanza ziara ya kikazi katika Mkoa wa Tabora ambapo atatembelea Wilaya zote saba (7) za Igunga, Nzega, Uyui, Sikonge, Kaliua, Urambo na Tabora .
Lengo la ziara ni kutembelea miradi mbalimbali ya maendeleo ili kujionea utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya mwaka 2015 ya Chama Cha Mapinduzi, kuhamasisha wananchi kushiriki shughuli za maendeleo na kutoa maelekezo kwa watendaji kuhusu masuala mbalimbali ya kiutendaji yatakayobainika katika ziara. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akivishwa skafu na kijana wa skauti mara baada ya kuwasili Igunga mkoani Tabora. (picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *