Mwanaharakati Mzalendo

Serikali ya Tanzania na Misri zinatarajia kusainiana mkataba wa makubaliano wa kuanzisha mashamba makubwa ya pamoja kwa lengo la kuinua kilimo cha ngano, mpunga na pamba Waziri wa Kilimo Mhe.
Japhet Hasunga akimkaribisha Waziri wa Kilimo na Ardhi wa Misri Mhe.
Dkt. Ezzidine Abu Stiet mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa
Dodoma kwa ajili ya mazungumzo na Mwenyeji
wake

 Waziri wa Kilimo Mhe.
Japhet Hasunga akiwa sambamba na Waziri wa Kilimo na Ardhi wa Misri Mhe.
Dkt. Ezzidine Abu Stiet wakiongoza kikao kazi kati ya Wataalam wa
Wizara ya Kilimo Tanzania na Wataalam wa Wizara
ya Kilimo ya Misri katika Ukumbi wa Wizara (Kilimo IV) Jijini Dodoma
Waziri
wa Kilimo Mhe. Japhet Hasunga akiwa sambamba na Waziri wa Kilimo na
Ardhi wa Misri Mhe. Dkt. Ezzidine Abu Stiet wakati wa majadiliano
na Wataalam kutoka Wizara ya Kilimo Tanzania na Wataalam wa Wizara ya
Kilimo ya Misri katika Ukumbi wa Wizara (Kilimo IV) Jijini Dodoma


Serikali
ya Tanzania na Misri zinatarajia kusainiana mkataba wa makubaliano wa
kuanzisha mashamba makubwa ya pamoja kwa lengo la kuinua kilimo cha
ngano, mpunga na pamba


Hayo
yamebainishwa na Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga mara baada ya kufanya
mazungumzo na timu ya Wataalamu wa kilimo kutoka Misri wakiongozwa na
Waziri wa Kilimo na Ardhi wan chi hiyo,
Dk Ezzidine Abu Stiet.


Mhe.
Hasunga amesema katika mazungumzo hayo wamekubaliana kushirikiana katia
Sekta ya Kilimo husan katika mazao ya mpunga, ngano na pamba ambapo
tande zote mbili zitakuwa na mashamba ya
pamoja.

“Kama
mnavyojua Misri wamepiga hatua katika kilimo hususani kilimo cha
umwagiliaji na tekinolojia hivyo tumekubaliana mafaniko hayo yahamie
hapa nchini.”

Waziri
Hasunga aliongeza: “Baada ya mazungumzo ya kina na makubaliano katika
maeneo ya ushirikiano, tumepeana miezi miwili ili ifikapo mwezi Mei
mwaka huu, tutasaini mkataba wa makubaliano
na kuanza utekelezaji.

Amesema
eneo lingine ambapo wamekubaliana ni kuimarisha Vituo vya Utafiti wa
mazao ili kupata mbegu bora na namna bora ya kuzitumia mbegu hizo na pia
kuhamisha ujuzi na zana kutoka Misri
ambao utasidia kuinua kilimo hapa nchini.

Waziri
Hasunga alisema kwa sasa Wataalam wa kilimo wa nchi hizo mbili
watatumia muda huu wa miez miwili kutembelea maeneo mbalimbali ili
kubainisha maeneo ambayo yanafaa kwa kilimo.

“Mfano
tuliwaza kupeleka kilimo cha ngano wilayani Misenyi mkoani Kagera
lakini wamesema eneo hilo ni dogo, hivyo wataalamu wa Misri na wale wa
Tanzania watapita maeneo mbalimbali kuangalia
maeneo yanayofaa na baadaye tusainiane mkataba wa makubaliano,”
alisema.

Naye
Waziri wa Kilimo na Ardhi wa Misri, Stiet alisema wamekuwa na
mazungumzo mazuri na yenye mafanikio na kukubalianakushirikiana katika
mafunzo, utafiti na tekinolojia katika sekta ya
kilimo ili kuboresha mazao ya kimkakati ya pamba, mbunga na ngano..

“Makubaliano
hayo yanaongeza wigo wa ushirikiano kati ya nchi hizi mbili ambayo ni
ya muda mrefu, tumekubaliana kuinua kilimo katika mazao matatu kwa
manufaa ya wananchi wa Tanzania. Baada
ya kusainiana mkataba tunategemea utekelezaji wa haraka,” alimalizia.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *