Sitoacha kufanya siasa hadi wapinzani watakapo nielewa – Maalim SeifKatibu Mkuu wa Chama cha Wananchi CUF, Maalim Seif Sharif Hamad amesema hatoacha kufanyakazi ya siasa hadi pale wapinzani wake watakapo muelewa kuwa yeye ni fundi wa siasa.


Kauli hiyo ameitoa wakati wa Mkutano Maalum wa Jumuiya ya wanawake CUF (JUKECUF) uliofanyika katika ukumbi Mjid kiembe samaki Mjini Unguja,

Mkutano huo ulikuwa na lengo kula kiapo cha utii kutoka kwa kina mama dhidi ya maamuzi ambayo yatatolewa na viongozi wao mara baada ya hukumu ya kesi zilizoko Mahakamani.

Maalim Seif alieleza kuwa kuna Viongozi wakubwa ndani ya CCM wanafikiria kuwa yeye ameisha kisiasa na hana nafasi tena katika ulimwengu wa siasa, jambo ambalo alieleza kuwa yeye yuko makini na hakuna kiongozi yoyote wa Chama cha Mapinduzi ambaye anaweze kueleza chochote mbele yake,

“Na wafanye tu mambo yao lakini mwaka huu watamjua ni nani Seif kwa kitu ambacho nitawafanyia,” alieleza Maalim Seif.

“Wamenichezea kwa muda mrefu lakini nasema sasa basi, wasubiri waone kitu ambacho nitawafanya mwaka, mchezomchezo basi” alisema.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa JUKECUF, Bi Fatma Ferrej alisema wanawake wote wa Zanzibar wakotayari kwa lolote lile ambalo viongozi wao watawateremshia mara baada ya kesi zao kumalizika.

“Sisi wanawake tunakuambia Maalim ulipo tupo na chochote utakachotuletea ndio tutakachopokea, hakuna kurudi nyuma,” alieleza Bi Fatma.

Alieleza kuwa wanawake hawanatabia ya kukata tamaa na kufahamisha kuwa wao hawako tayari kuwaacha viongozi wao pekeyao.

Aliishtum CCM kwa kuingiza mgogoro ndani ya chao na kudai kuwa wala wasidhani wamefanikiwa na badala yake alisema wanakuja kivyengine kabisa.

Mapema wakisoma risala yao wanawake wa wilaya 11 za Zanzibar wamesema kuwa na kiongozi wao Katibu Mkuu malim seif kwa muda wa mika 27 sasa katika harakati ya kupigania Demokrasia ya kweli katika visiwa vya Zanzibar.

“Tunakujua na kukufahamu vyema umekuwa muaminifu kawetu nasi tumejenga utiifu kwako na kwa chama chetu cha CUF kwetu sisi wewe ni shujaa wetu usiyeyumba kupigania kile tunachokiamini ndio mana nasi mapenzi yetu hayayumbi kwako.”

Pia risala hiyo imeleza pamoja na mamuzi ya kesi zote zilizopo mahakamani zilizofunguliwa na chama hicho wako pamoja na viongozi wao kwa lolote lile litakaloamuliwa na viongozi hao.

“Kamwe hatutohadaiwa na wasiokipendelea mema chama chetu kwani tunafahamu kwamba tuna lengo ambalo hatujalifikiana viongozi pekeea watakoweza kutufikisha Tanzania kwenye Demokrasia ya kweli ni viogozi wa chama cha CUF tunachohitaji ni kauli yako,” ilieleza risala hiyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *