Mwanaharakati Mzalendo

BAADA YA SIKU 31 TU KUPITA, PAUL SCHOLES AJIUZULU UKOCHA OLDHAM ATHLETIC

Aliyewahi kuwa mchezaji mashuhuri wa klabu ya Manchester United Paul Scholes, amejiuzulu kufundisha klabu ya Oldham Athletic baada ya mechi saba tu akiwa madarakani katika ligi daraja la pili nchini Uingereza. 
Kiungo huyo wa zamani wa Manchester United na Uingereza aliichukua Oldham Februari 11 na kuondoka klabuni hapo baada ya siku 31 tu ndani ya Boundary Park. 
Scholes alishinda mechi yake ya kwanza katika klabu hiyo ya kitaani kwake lakini akapata sare tatu na kufungwa tatu. 
Scholes amedai kwamba ahadi alizopewa kabla ya kusaini mkataba ili aweze kuingoza klabu vizuri hazijatimizwa. 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *