Mwanaharakati Mzalendo

BAADA YA TIMU ZAO KUTOLEWA, NEYMAR NA RAISI WA ROMA WAIPONDA V.A.R NA KUILALAMIKIA

Mchezaji nyota wa klabu ya PSG, mbrazil NEYMAR, ameonyesha kukerwa na maamuzi yaliyotolewa dakika za mwisho za nyongeza za mchezo wao dhidi ya Manchester United yaliyozaa penati ambayo ikawapa ushindi Man United na kuwapeleka Manchester United katika hatua ya robo fainali. 
“Hii ni aibu, wameweka watu wanne ambao hawajui chochote kuhusu soka ndio wawe wanaangalia marudio ya video ya VAR. Hakuna penati pale. Inawezekanaje awe ameshika wakati mpira umemgonga kwa nyuma” Aliandika Neymar huku mwisho akamalizia na tusi. 
Wakati hilo la Neymar likitrend, naye Rais wa klabu ya AS Roma, James Pallotta hakusita kuelezea hisia zake za kuumizwa na maamuzi ya VAR. 
“Mwaka jana tuliiomba VAR kwenye Ligi ya Mabingwa kwasababu kwenye hatua ya nusu fainali tulionewa na usiku wa leo VAR ipo lakini bado tumeibiwa. Ni wazi kabisa Patrik Schick aliangushwa ndani ya Boksi, VAR inaonesha hilo na hakuna kilichopatikana. Nimechoka na huu uchafu. Nimekata tamaa.” Alimalizia raisi huyo. 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *