Mwanaharakati Mzalendo

BUFFON: MLINDA MLANGO ASIYE NA BAHATI KATIKA LIGI YA MABINGWA BARANI ULAYA

Katika maisha ya soka kumekuwa na changamoto nyingi za hapa na pale mpaka ufikie malengo yangu au kiujumla. Maisha ya soka ni mafanikio ambayo leo hii utakumbukwa duniani na watu na itabaki kudumu milele na milele.
Ukiongelea moja ya makipa bora duniani huwezi kuliacha kutaja jina la goli kipa mkongwe Gianluig Buffon, moja ya makipa bora duniani kwa sasa wenye uwezo mkubwa na hata pia ni kiongozi akiwa uwanjani kwa maana ya kuwaongoza wenzake nini cha kufanya.
Buffon, ni moja ya makipa ambayo amekuwa hana bahati na kutwaa taji la michuano ya klabu Bingwa Barani Ulaya ndo kitu peke kinachomfanya mpaka leo asistafuu soka na kuamini kuwa ipo siku atashinda michuano hiyo? Kwa mara ya kwanza katika historia yake binadamu tunaishi kwa ndoto na kujituma kila kukicha ili tuweze kufanikiwa katika maisha .
Fainali ya mwaka 2003 pale katika dimba la Old Trafford kati ya Ac Milan dhidi ya Juventus, Buffon, alikuwa ni goli kipa wa Juventus, walipoteza kwa mikwaju ya penati .
Msimu wa mwaka 2015 walifika fainali tena kwenye michuano hiyo akiwa Juventus,walipoteza mbele ya Barcelona, kwa mabao 3-1.
Msimu wa mwaka 2016 walipoteza fainali ya klabu Bingwa Barani Ulaya kwa mabao 4-1.
Ukiangalia fainali zote aliopoteza Buffon, sio kama hana timu nzuri bali wanakutana na timu bora zaidi yao?ukirudi kwenye msimu wa mwaka 2016 wanamtoa Barcelona, kwenye hatua ya nusu fainali Barcelona ilikuwa inaundwa na MSN , Messi Suarez, na Neymar walikuwa kwenye ubora waliwasimamisha kwa dakika 180 wasiruhusu kupata bao?wengi waliamini kuwa huo mwaka wa Buffon, lakini mambo yalienda hovyo. 
Juventus ya msimu huo ilikuwa ina safu bora ya Ulinzi kwa maana ya BBC Bonucci, Brazagli, na Chiellin, walijikuta fainali wakipoteza mbele ya Real Madrid chini ya Cristiano Ronaldo. 
Buffon, aliamini katika imani yake aondoke Juventus,akatafuta changamoto nyengine ametua Paris Saint Germain, wametupwa nje kwenye michuano hiyo hatua ya 16 bora na Manchester United. 
 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *