Mwanaharakati Mzalendo

CHARZ BABA AFUNGUKIA ISHU YA KUOA MPENZI WA ALIKIBA

Msanii wa muziki wa dansi kutoka bendi ya Twanga Pepeta, Charz Baba amefungukia ishu ya kuoa mke ambaye inadaiwa kuwa alikuwa ni mpenzi wa msanii wa bongo fleva Ali Kiba.

Charz amesema hajui chochote kuhusu mahusiano ya zamani kati ya mke wake aliyemuoa mwaka jana na msanii Ali Kiba, anachokijua yeye ni kwamba mke wake na familia ya Kiba zina ukaribu na ndio maana hata katika harusi ya mdogo wake Ali, Zabibu Kiba, mwanadada huyo alikuwa mtu wa karibu sana katika kukamilisha harusi hiyo.

“Nimeamua kufunika kombe ili mwanaharamu apite na ukitaka kumchunguza bata utashindwa kumla utaishia kutapika,mapenzi yanamambo mengi sana ukitaka kuyafatilia yote huwezi kukaa kwenye ndoa mimi na mke wangu kila mtu anamadhambi yake ila tulikaa chini tukaamua kuachana na ya nyuma na kuanzia familia yetu”, amesema Charz Baba.

Pia Charz alimalizia kwa kusema kitendo cha Ali Kiba kuja na kuimba kwenye harusi yake hiyo inadhihirisha wazi kwamba roho yake ni nyeupe na hana tatizo lolote na mke wake hivyo kwa sasa wanaishi na mke wake kwa upendo na amani na hakuna kati yao anayeangalia historia ya zamani ya kimapenzi kati yao.

Imedaiwa kuwa mwanadada huyo huenda angeolewa na Alikiba endapo asingekwenda kuoa Mombasa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *