Mwanaharakati Mzalendo

CLAUDIO RANIERI ATEULIWA KUWA KOCHA WA AS ROMA MUDA MFUPI BAADA YA KUTIMULIWA FULHAM

Kweli “fundi halali njaa”. Huu ndio msemo thabiti kabisa kuutumia katika maisha ya kocha Claudio Ranieri ambaye amekuwa akipata kazi na kufukuzwa mara kwa mara. Wiki 2 nyuma alikuwa kocha wa Fulham Fc ya ligi kuu ya Uingereza na akafukuzwa kutokana na matokeo mabovu timu yake iliyokuwa inayapata. 
Sasa baada ya Alhamisi klabu ya AS ROMA ya Italia kumfukuza kazi aliyekuwa kocha wao Eusebio De Francesco baada ya kipigo cha 3-1 dhidi ya PORTO kwenye ligi ya mabingwa Ulaya, Jana wamemteua Claudio Ranieri kuwa kocha wao mpya mpaka Juni 2019.
Ranieri a.k.a The Tinker Man, alipata mafanikio makubwa sana na klabu ya LEICESTER CITY msimu wa 2015 kwa kuchukua ubingwa wa ligi kuu ya Uingereza lakini uliofuatia alifukuzwa na kujiunga na Nantes ya Ufaransa kabla ya kufukuzwa tena na kujiunga na Fulham. 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *