Mwanaharakati Mzalendo

HARMONIZE AMKOSA WIZKID

NYOTA wa muziki wa kizazi kipya nchini, Rajab Kahal ‘Harmonize’, amesema kushindwa kwa staa wa Nigeria, Wizkid, kuingiza mashairi kwenye ngoma yake mpya kumetokana na kutingwa na majukumu aliyokuwanayo.

Ngoma hiyo mpya  inayokwenda kwa jina la ‘Kainama’, imenogeshwa sauti na nyota Burna Boy ambapo imeanza kufanya vyema sokoni.

Harmonize amesema awali Wizkid alitakiwa kuingiza baadhi ya mashairi lakini alibanwa na majukumu na nafasi yake kuzibwa na Burna boy.

“Ni wimbo ambao awali alitakiwa kuwepo Wizkid, lakini tulimwelewa baada ya kubanwa na majukumu.. nashukuru nafasi yake kaicheza vyema Burna boy,” alisema Harmonize.

OMMY DIMPOZ AMCHUKULIA POA STEVE NYERERE

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *