Mwanaharakati Mzalendo

HAYA NDIO MAHITAJI YA OLE GUNNAR SOLSKJAER KWENYE DIRISHA KUBWA LA USAJILI

Kwa mujibu wa Metro, Ole Gunnar Solskjaer amefanya mazungumzo na bodi ya Manchester United jijini London mwezi uliopita ambapo alielezea mipango yake ya msimu ujao. 
Ameripotiwa kuiambia Bodi kwamba anahitaji beki wa kulia, beki wa kushoto, winga wa kulia, beki wa kati na kiungo mshambuliaji. 
Mabeki wa pembeni Antonio Valencia na Matteo Darmian wanatarajiwa kuondoka klabuni mwishoni mwa msimu huu huku winga wa kulia imekuwa kipaumbele kabla ya hata Jose Mourinho kuondoka klabuni. 
Kiungo mwingine mshambuliaji ni kwa ajili ya kuongeza ushindani na mbadala wa Paul Pogba pale anapokosekana kikosini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *