Mwanaharakati Mzalendo

KIPA OSPINA AWATOA HOFU MASHABIKI WA NAPOLI KUHUSU AFYA YAKE

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Golikipa wa Napoli David Ospina ametoa shukrani na kuthibitisha kuwa anaendelea vizuri na matibabu akiwa nyumbani.
Golikipa huyo alipoteza fahamu na kuanguka gafla dakika ya 42′ katika mchezo wao dhidi ya Udinese wikiendi hii na kuwahishwa katika hospitali kubwa ya karibu.
Awali katika dk 10 za mwanzo wa mchezo Ospina alipata jeraha la kichwa baada ya kugongana na mshambuliaji Pussetto wa Udinese lakini alitibiwa na kuendelea kucheza.
Inaaminika Ospina alipata ‘Concussion’ kutokana na majeraha hayo ya kichwa na ndio yaliyopelekea yeye kuanguka na kupoteza fahamu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *