Mwanaharakati Mzalendo

MANCHESTER CITY WAZIDI KUANDAMWA, TUHUMA HIZI MPYA ZAIBULIWA.

Manchester City wamegoma kutoa tamko lolote kuhusu tuhuma mpya za kuvunja kanuni za FFP kwa mujibu wa taarifa kutoka Sky sports.
Jarida la Ujerumani Der Spiegel wameibua ujumbe wa barua pepe ( emails ) ambazo zimevuja ambazo zinaonesha mmiliki Sheikh Mansour aliweka fedha zake binafsi moja kwa moja kwenye klabu ili kuongezea juu yake fedha walizopata kutokana na wadhamini na kuiwezesha City kukidhi mahitaji ya FFP.
Kanuni za UEFA zimeweka kiwango cha fedha ambacho mmiliki anaruhusiwa kuingiza kwenye klabu na Mansour kupitia mfuko wake wa uwekezaji – Abu Dhabi United Group , anatuhumiwa kuzidi kiwango hiko.
Kwa kujibu kuhusu email hizo ambazo zimevuja, City wamesema: “Hatutoa tamko lolote kuhusu nyaraka zozote ambazo zimearifiwa kudukuliwa au kuibiwa kutoka City Football Group na mfanyakazi wa City na mtu yoyote anayehusika na City. Jaribio la kutaka kuharibu heshima ya klabu inaonekana wazi”
City tayari wanachunguzwa na UEFA kuhusu emails ambazo ziliwekwa hadharani na jarida la Der Spiegel mnamo mwaka jana kuhusu kuvunja kanuni za FFP.
Wakati huo huo , Der Spiegel waliwatuhumu City kwa kushindwa kutoa taarifa hadharani kuhusu mchezaji wao kwa kipindi hiko Bruno Zuculini kwamba alikiwa ana milikiwa na upande wa tatu kitu ambacho hakiruhusiwi chini ya kanuni cha FA .
Msemaji wa FA amesema, “tulikuwa tunajua kuhusu tuhuma hizo na tunazifanyia kazi”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *