Mwanaharakati Mzalendo

‘PSG YA MAKARATASI’ YACHAPWA NYUMBANI NA ‘WATOTO WA OLE’, NGOME YA ROMA YAANGUSHWA NA PORTO KATIKA USIKU WA ULAYA.

Wakati bado hatujasahau na tunaongelea yaliyotokea jana kwa waliokuwa mabingwa watetezi mara tatu mfululizo Real Madrid pale kwao Bernabeu, jana yameibuka mengine bwana. PSG ikiwa na advantage ya kuongoza magoli 2-0 imefungwa 3-1 na kutolewa nje ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya. 
Utakubaliana na mimi kuwa wengi wetu hatukuipa nafasi Manchester United ambayo ilikuwa ikiandamwa na majeruhi wengi kuliko PSG na pia walikuwa wanamkosa kiungo mchezesha timu Paul Pogba. Kingine ni kuwa walikuwa wanaenda nyumbani kwa PSG, uwanja wa Parc de France kitu ambacho kingeongeza ugumu wa wao kufanya maajbu. 
Lakini acha mpira uitwe mpira tu. Dakika ya pili tu, Romelo Lukaku akalianzisha kwa kufunga goli la kwanza. Ikumbukwe kuwa kocha wao OleGunnar Solskjaer katika mkutano wake na waandishi wa habari kabla ya mchezo alisema “tunahitaji goli la kuongoza tu kwanza ndipo mengine yafuate. Tukilipata mapema basi chochote chaweza kutokea.” Na kweli maajabu yametokea. 
Dakika ya 12 beki wa kushoto wa PSG Juan Bernat akaisawazishia PSG na matokeo kuwa 1-1 (agregate 3-1). Lakini wachezaji wa Man United waliendela kutafuta namna ya kushinda hiyo mechi na ndipo bwana Lukaku alipofumania nyavu tena dakika ya 30 na kufanya matokeo yawe 1-2 (aggregate 3-2). Mpaka mapumziko, ilikuwa PSG 1-2 Man United. 
Kipindi cha pili kila timu ilikaza kwelikweli lakini Manchester United walikuja kupewa penati mnamo dakika ya 93 (muda wa nyongeza) na Marcus Rashford hakukosea. Akafunga penati hiyo na kufanya matokeo yawe 1-3 (aggregate 3-3) na Man United wakafuzu kuingia robo fainali kwa magoli mengi ya ugenini. 
PSG ni timu laini (ya makaratasi) isiyoweza kupambana kila inapofika hatua hizi kwani mwaka 2017 mwezi March tarehe 8 walichapwa 6-1 na FC Barcelona na kupoteza advantage ya magoli 4-0 waliyofunga kwenye mechi ya kwanza. Jana March 6 wanachapwa 3-1 na Man United na kupoteza advantage ya 2-0 waliyoipata katika mechi ya kwanza. 
Upande wa pili katika mechi nyingine ilishuhudia AS ROMA waliokuwa na advantage ya ushindi wa mechi ya kwanza wa 2-1 dhidi ya FC PORTO, jana wakachapwa 3-1 na kutolewa nje katika michuano hiyo. 
Francisco Soares wa Porto alifunga goli la kwanza dakika ya 26 lakini mkongwe wa Roma, Daniele De Rossi alisawazisha dakika ya 37 kwa mkwaju wa penati. Alikuwa ni Mousa Marega ambaye alifunga katika mechi ya nane mfululizo katika Uefa Champions League, alifunga dakika ya 52 na kufanya aggregate kuwa 3-3 na kulazimisha waende Extra Time. 
Na katika muda huo wa nyongeza ndipo Alex Telles alipopigilia nyundo ya mwisho dakika ya 117 kwa penati na kuiangusha ngome ya ROMA. Uefa Champions League itaendelea wiki ijayo siku za Jumanne na jumatano. 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *