Mwanaharakati Mzalendo

Rais Magufuli Amtaka IGP Sirro Kutowarudisha Makao Makuu maofisa wanaoshindwa kufanya vizuri katika vituo vyao


Rais Magufuli Amtaka IGP Sirro Kutowarudisha Makao Makuu maofisa wanaoshindwa kufanya vizuri katika vituo vyao

Rais Magufuli amemtaka Mkuu wa Jeshi la Polisi, Simon Sirro, kutowapeleka Makao Makuu wa jeshi hilo maofisa wanaoshindwa kufanya vizuri katika vituo vyao.

Akizungumza baada ya kuwaapisha mawaziri wawili Ikulu jijini Dar es Salaam leo Jumatatu Machi 4, Rais Magufuli pia amemtaka Sirro kutoogopa kuleta majina ya watu ambao wanatakiwa kupunguziwa vyeo.

“Nakuomba IGP, watu ambao wanaoshindwa ‘kuperfom’ wasiwe wanapelekwa makao makuu, mpeleke hata akawe  chini ya RPC mwingine huko .

“Pia usiogope kuleta makamishna ambao unataka tuwapunguze hata nyota zao wala usisite kwa sababu tumezoea kutoa nyot, tu sasa tutazichukua…” amesema Rais Magufuli.

Aidha, akizungumzia kuhusu rushwa, amesema watu wasitegemee kupata vyeo kwa sababu ya rushwa bali atapata cheo kwa sababu ya utendaji wake.

“Tumekaa Mwanza kule kuna ushahidi wa kutosha kwamba wale polisi walihusika kusindikiza ile dhahabu na wakahongwa mamilioni ya fedha.

“Inapofikia wanajeshi wanahongwa mamilioni ya fedha kunakuwa na hitilafu, niwaombe makamishna tujenge jeshi la polisi kama lilivyoanzishwa na Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, wale wachache wanaolichafua waonyeni ikishindikina kuonywa basi waondoeni,” amesema Rais Magufuli.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *