Mwanaharakati Mzalendo

TETESI ZA USAJILI: UMTITI KUTUA MANCHESTER MAJIRA YA KIANGAZI

Jarida la Italia Calciomercato pamoja na la Hispania AS, yamedai kwamba Barcelona wapo tayari kumuuza beki Samuel Umtiti katika dirisha la usajili la majira ya kiangazi. 
Beki huyo wa kimataifa wa Ufaransa ambaye mkataba wake unafikia kikomo mwaka 2023 ameripotiwa kuvutiwa na vilabu vyote viwili Manchester United na Manchester City, vilabu viwili ambavyo amewahi kuhusishwa navyo. 
Umtiti mwenye umri wa miaka 25 alijiunga na Barcelona kwa dau la Pauni Milioni 21.5 kutoka Lyon mwaka 2016 siku zake huenda zikahesabika kama mabingwa wa Hispania wakimnasa Matthijs de Ligt kutoka Ajax. 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *