Mwanaharakati Mzalendo

VIRGIL VAN DJIK ATOA ANGALIZO KWA WACHEZAJI WENZAKE KUELEKEA MECHI YAO NA BAYERN

Beki kisiki wa klabu ya Liverpool Virgil Van Dijk amewaonya wenzake kuwa makini sana klabu ya Bayern ambao wanatarajia kuvaana nao hapo kwenye mchezo wa marudiano ya klabu bingwa kule Allianz Arena Ujerumani.
Mchezo wa kwanza ulishuhudia miamba hao wa soka barani ulaya kutoka sare tasa kunako dimba la Anfield.
Van Dijk amewamwagia sifa kemkem mabeki wa klabu ya Bayern kwa kuweza kusimama imara.
“Mchezo wa kwanza ulikuwa mgumu sana. Mipango yetu kuipenya safu yao ya ulinzi ilikwama. Lakini hata wao walituheshimu sana kwa kucheza kwa tahadhari kubwa”
Mtazamo wake kuhusiana na mchezo ujao Van Dijk ana mtazamo gani?
“Ni mchezo kuvutia sana. Timu zote zina uwezo. Tunajua watacheza kwa kujiamini. Watatumia nguvu kubwa ili wapate matokeo”
“Kama tunahitaji kushinda ni lazima tucheze vyema zaidi kuliko tulivyocheza hapo awali.”
Vipi mwenendo wa klabu kwa ujumla kwenye michuano ya klabu bingwa?
“Kwenye michezo ya makundi tulisuasua sana licha ya kupita. Hatukuwa na msururu mzuri wa matokeo hasa mechi za ugenini”
“Bado tuna imani kubwa na klabu yetu hasa baada ya kujitahidi kutokuruhusu bao mchezo uliopita”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *