Mwanaharakati Mzalendo

DIAMOND ATOBOA KISA CHA ‘KUTELEKEZA’ WATOTO WAKE

Staa wa Bongo Movie, Diamond Platnumz ametoboa sababu ya kuwatelekeza watoto wake wawili, Latifah na Nillan wanaoishi nchini Afrika Kusini kwa madai kuwa mzazi mwenzake hampi ushirikiano.

Akizungumza jana Aprili 23, mwaka huu katika kituo cha televisheni Wasafi, Diamond alisema kwa takribani miezi mitatu sasa amesitisha kutoa matunzo ya watoto kwa kuwa mzazi mwenzake, Zari hampi ushirikiano ikiwamo kuwaleta watoto nchini.

Diamond amesema kila mwezi alikuwa akitoa dola za Marekani 2,000 ambazo ni wastani wa Sh5 milioni kwa ajili ya matunzo ya watoto.

“Niseme ukweli kabisa, nina kama miezi mitatu hivi sijapeleka fedha za matunzo ya watoto kwa sababu mwenzangu hataki hata niongee na watoto, hebu fikiria hata kupitia mfanyakazi wa ndani amegoma nisiongee nao,” amesema.

Ameeleza kuwa amefanya jitihada za kila namna kuhakikisha anawasiliana na watoto wake lakini mwanamke huyo mwenye asili ya Uganda amemuwekea ngumu.

“Nilijaribu kuwasiliana na mtoto wake wa kiume, yule mkubwa (wa Zari) lakini mwenzangu ameniwekea ngumu,” amesema.


Jitihada nyingine anazosema mwenzake amekuwa akizizima ni za kuwaleta watoto nchini akisema amemuwekea masharti kuwa lazima aje nao.

“Zari anataka aje na watoto, mimi nimemwambia mama nina mahusiano mengine nikamshauri mama yangu mzazi awafuate watoto lakini akakataa akasema labda niende kuwaangalia Sauzi (Afrika Kusini),” amesema.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *