Mwanaharakati Mzalendo

KHADIJA KOPA AJIPANGA KUSTAAFU MUZIKI

Mwimbaji mkongwe wa Taarabu hapa nchini, Khadija Omar Kopa ‘MAlkia wa Mipasho’ amesema anajiandaa na maisha akistaafu kuimba na ameshaanza maandalizi kwa kujikita kwenye biashara.

Kopa ambaye ni mmoja ya waasisi wa muziki wa taarabu ya kisasa, amesema licha ya muziki huo kumweka kwenye ramani nyingine ya maisha, lakini anaamini wakati wowote kuanzia sasa anaweza kustaafu.

“Kuna kipindi nitaachana na muziki, lakini kwa sasa nimeamua kujiwekeza kwenye biashara, natamani sana kuzoea biashara nje ya muziki kwa kuwa najua sitaweza kukaa maisha mengine bila kujishughulisha,” alisema Kopa.

Alisema moja ya vitu vilivyomfanya kumudu kwenye muziki wake hadi sasa akiwa na jina ni pamoja na kujiongeza zaidi na kuwa mbunifu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *