OMMY DIMPOZ AFUNGUKA KUHUSU ‘BIFU’ NA DIAMOND PLATNUMZ

Mkali wa wimbo ‘You Are The Best’  unaotikisa anga la Bongo Fleva, Ommy Dimpoz amesema hana tatizo na msanii mwenzake  Diamond Platnumz na kuweka wazi kuwa kilichowatenganisha ni kuwa chini ya usimamizi tofauti wa kazi zao.
“Kilichopo sasa ni mimi kuwa chini ya usimamizi wa Rock Star nayeye kuwa kwenye lebo yake ya WCB, hicho ndiyo kinacho tutofautisha  na sio kingine”
Ommy ameyasema hayo wakati akizungumza na gazeti la mwanaspoti hivi karibuni.
Akiweka wazi kuwa hajawahi kufikiria kugombana na nyota huyo na siku ikitokea wanaweza kufanya kazi paomja .
“Ikitokea nahitaji kufanya kazi naye nitafanya hivyo ila kwasasa acha maisha yaendelee na nawaomba mashabiki watambue kuwa sijawahi kugombana naye na sifikirii kuwa na ugomvi na msanii ambaye tunafanya kazi aina moja” alisema Ommy
Akizungumzia ngoma yake mpya hiyo ya YOU ARE THE BEST alisema kuwa anamshukuru Mungu Inaendelea kufanya vizuri na mashabiki wameipokea vizuri tafauti na vile alivyodhani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *