Mwanaharakati Mzalendo

TETESI ZA USAJILI: MAN UNITED HATARINI KUWAPOTEZA MATA NA HERERA DIRISHA LA KIANGAZI

Klabu ya Manchester United wapo hatarini kuwapoteza wachezaji wao nyota Ander Herrera na Juan Mata kwa wapinzani wao wa barani Ulaya na wote kwa uhamisho huru. 
Herrera ameripotiwa kukubali dili la kuhamia Paris Saint-Germain na Mata ameripotiwa kuwa kwenye mazungumzo ya kuhamia FC Barcelona kwa mujibu wa taarifa kutoka shirika la habari la Sky Sports. 
Wahispania hao wawili wamekuwa huru kuongea na vilabu vya nje ya Uingereza tangu Januari mosi kwasababu mikataba yao inafikia tamati mwezi Juni mwaka huu na hakuna dalili ya kupewa mikataba mipya. 
Manchester United wamekuwa kwenye mazungumzo ya kuhusu mikataba mipya kwa wachezaji hao wote wawili kwa miezi kadhaa sasa, na kutoka upande wa United mazungumzo yanaendelea lakini bado hakuna kilichoamuliwa mpaka sasa. 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *