USIKU WA ULAYA: BARCA WAMCHINJA UNITED, VIJANA WA AJAX WAMFANYA MBAYA BIBI KIZEE WA TURIN – Mwanaharakati Mzalendo
ADVERTISEMENT
  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Mwanaharakati Mzalendo
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
No Result
View All Result
Home AJAX

USIKU WA ULAYA: BARCA WAMCHINJA UNITED, VIJANA WA AJAX WAMFANYA MBAYA BIBI KIZEE WA TURIN

I am Magnifico by I am Magnifico
Apr 17, 2019
in AJAX, COUTINHO, CRISTIANO RONALDO, DE LIGT, FC BARCELONA, JUVENTUS, Lionel Messi
0 0
0
USIKU WA ULAYA: BARCA WAMCHINJA UNITED, VIJANA WA AJAX WAMFANYA MBAYA BIBI KIZEE WA TURIN
0
SHARES
62
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter
Nyota wa FC Barcelona Lionel Messi (kushoto) na Philipe Coutinho wakishangilia moja ya magoli waliyoyafunga hapo jana katika mchezo wao dhidi ya Manchester United pale CAMP NOU. 

Usiku ambao mechi za Ligi ya mabingwa wa Ulaya zinachezwa huitwa USIKU WA ULAYA kwasababu ni muda ambao ligi zote husimama, macho na masikio yote huelekezwa kwenye mechi hizo. Shangwe na msisimko wa ajabu hutokea pindi mechi izo zinapochezwa na mashabiki hujaza viwanja vya mechi hizo na pia duniani kote watu hufuatilia kupitia Luninga na simu zao.

Sasa jana kulikuwa na mechi 2 ZA MUHIMU kwa kila timu katika hatua ya robo fainali. Kule Hispania, FC Barcelona ilikuwa ikiwakaribisha Manchester United kutoka Uingereza huku matokeo ya mechi ya kwanza iliyochezwa pale Old Trafford Uingereza, Barca waliifunga Man United 1-0. Kule Italia katika jiji la Turin, Juventus FC walikuwa wakiwakaribisha madogo wa Ajax Amsterdam huku matokeo ya mechi ya kwanza iliyochezwa kule Uholanzi yakiwa ni 1-1.

Mpaka dakika 25 inafika katika mchezo wa kule Hispania, FC Barcelona walikuwa wakiongoza kwa mabao 2-0 na aliyekuwa kafunga ni si mwingine bali Mfalme wao LIONEL MESSI huku akimuacha golikipa David Degea akihuzunika mno.

Kule Italia, mpaka HALF TIME inafika ilikuwa ni bao 1-1 huku “mwenye Champions league yake” mreno CRISTIANO RONALDO akifunga kwa kichwa dakika ya 28 na baadaye Donny Van De Beek kusawazisha dakika ya 34.

Mpaka hapo watu wengi tuliitoa Man United kwenye michuano hii na tukabaki na mechi ya Juve Vs Ajax ambapo tulikuwa tunasubiri tuone CR7 kama atafanya maajabu yake tena na kuibeba Juve mgongoni kuipeleka hatua ya nusu fainali.

Mambo hayakuwa rahisi kama tulivyodhani kwa Ajax nao walionekana kutaka kwenda nusu fainali na hawakuonyesha kuchoka wala kukata tamaa. Na ndipo dakika ya 67 beki na nahodha wa AJAX, kinda Matthijs De Ligt akafunga goli la pili kwa Ajax ambalo liliongeza kazi mara mbili kwa Juve kwani iliwabidi wafunge magoli mawili zaidi ndio wapite kwani droo ya 2-2 isingewapitisha.

Juve walihaha mno uwanjani kwao pale lakini Ajax waliendelea pia kushambulia na kuwafanya Juve wasijiachie sana kwenda mbele. Wanasema kwenye mpira wa miguu, njia nzuri ya kujilinda ni kushambulia.

Nahodha wa AJAX, Matthijs De Ligt (mwenye kitambaa mkononi) akishangilia goli lake hapo jana dhidi ya Juventus katika mchezo wa marudiano wa hatua ya robo fainali. Goli hilo ndio liliamua Ajax wasonge mbele hadi nusu fainali. 

Mpaka mpira unaisha matokeo yalikuwa ni Juventus 1-2 Ajax. Matokeo hayo yakawatoa Juventus nje ya mashindano ya ligi ya mabingwa Ulaya. Na mshambuliaji Cristiano Ronaldo akawa ameshindwa kufuzu hatua ya nusu fainali kwa mara ya kwanza tokea mwaka 2010.

Kule Hispania Messi alizidi kung’aa kwani alianzisha move ambayo ilimkuta Jordi Alba upande wa kushoto ambaye alienda nao kidogo na kuupiga uingie ndani lakini kwa nje ya box na ndipo ulipomkuta mchawi PHILIPE COUTINHO ambaye aliuweka sawa na kuachia KOMBORA ambalo Degea pamoja na umahiri wake woooote hakuweza kulifikia. Barca wakamaliza mechi hiyo kwa goli hizo 3.

Leo ni zamu ya TOTTENHAM VS MAN CITY (1-0), na LIVERPOOL VS PORTO (2-0). Nani anapita, nani anafungasha virago?

Tags: Manchester UnitedMICHEZOUEFA
ADVERTISEMENT
I am Magnifico

I am Magnifico

Related Posts

Sakata La Barca Na Atletico Kuhusu Usajili Wa Griezmann Limefikia Hapa
ANTOINE GRIEZMANN

Sakata La Barca Na Atletico Kuhusu Usajili Wa Griezmann Limefikia Hapa

by I am Magnifico
Sep 17, 2019
0

Kwa muda mrefu sasa kumekuwa na sakata...

Read more
Tetesi na Habari za Soka Barani Ulaya leo 13/09/2019

Tetesi na Habari za Soka Barani Ulaya leo 13/09/2019

Sep 13, 2019
Luis Enrique Afiwa Na Mtoto Wake wa Kike

Luis Enrique Afiwa Na Mtoto Wake wa Kike

Aug 30, 2019
Haya Ndio Makundi Ya Ligi Ya Mabingwa Ulaya 2019/20

Haya Ndio Makundi Ya Ligi Ya Mabingwa Ulaya 2019/20

Aug 30, 2019
Tetesi na Habari za soka Barani Ulaya leo 28/08/2019

Tetesi na Habari za soka Barani Ulaya leo 28/08/2019

Aug 28, 2019
Ronaldo Ataja Sababu Zinazomfanya Aone 2018 kuwa Mwaka Mbaya Zaidi Katika Maisha yake

Ronaldo Ataja Sababu Zinazomfanya Aone 2018 kuwa Mwaka Mbaya Zaidi Katika Maisha yake

Aug 22, 2019
Next Post
WATU 150 HAWAJULIKANI WALIKO BAADA YA BOTI KUZAMA ZIWA KIVU

WATU 150 HAWAJULIKANI WALIKO BAADA YA BOTI KUZAMA ZIWA KIVU

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

I agree to the Terms & Conditions and Privacy Policy.

Currently Playing

KRANTZ MWANTEPELE (FOUNDER & CEO)

ADVERTISEMENT

KONCEPT TV

https://www.youtube.com/watch?v=0HP0mB_rtIU&t=7s
ADVERTISEMENT
Mwanaharakati Mzalendo

Mwanaharakati Mzalendo ni mtandao namba moja kwa habari makini kutoka pande zote za dunia kuhusiana na Michezo, Siasa, Afya, Elimu, Mahusiano, Vituko, n.k

Wasiliana nasi kwa Email;krantzcharles@gmail.com
SIMU; 0658123310

Follow Us

April 2019
M T W T F S S
« Mar   May »
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
2930  
Currently Playing
  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

Login to your account below

Forgotten Password?

Fill the forms bellow to register

*By registering into our website, you agree to the Terms & Conditions and Privacy Policy.
All fields are required. Log In

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In