ARUSHA: SERIKALI YATAIFISHA MALI ZA WAKILI MWALE – Mwanaharakati Mzalendo
ADVERTISEMENT
  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Mwanaharakati Mzalendo
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
No Result
View All Result
Home Arusha

ARUSHA: SERIKALI YATAIFISHA MALI ZA WAKILI MWALE

I am Magnifico by I am Magnifico
May 6, 2019
in Arusha, HABARI TANZANIA
0 0
0
0
SHARES
58
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter
ADVERTISEMENT

Serikali imetaifisha rasimi Mali za Wakili maarufu Nchini Median Mwale zenye thamani ya Tsh bilioni 1.2 zilizotokana na zao la utakatishaji mara baada ya mahakama kuu kumtia hatiani na kuamuru Mali hizo zitaifishwe.
Akiongea katika zoezi la makabidhiano kati ya ofisi ya Mkurugenzi wa mashtaka DPP na Hazina,Mkurugenzi wa Mashtaka , (ASP )Biswalo Mganga alizitaja Mali hizo kuwa ni pamoja na Magari sita ya kifahari yanayoshikiliwa kituo kikuu cha polisi,jijini hapa.
Mali zingine zilizotaifishwa ni pamoja na Nyumba mbili ikiwemo iliyopo ploti Namba 261 block c Njiro na nyumba nyingine iliyopo ploti namba 22 iliyopo eneo la Ilikyurei ambayo ilikuwa mali ya Wakili Loomo Ojale na shamba moja la ekari 10 lililopo eneo la Ngaramtoni.
Alisema hatua hiyo imekuja kufuatia mahakama kuu kanda ya Arusha, kutaifisha Mali hizo na kwamba April 14,2019 mahakama hiyo ilitoa kibali cha kuzitaifisha rasimi na kuwa Mali ya serikali.
“Kwa mujibu wa sheria Mali zinapotaifishwa kuwa Mali ya serikali zinakuwa chini ya katibu mkuu Hazina” Alisema.
Naye kaimu mkurugenzi wa idara ya usimamizi wa Mali za serikali Hazina,Benezeth Rutta Alisema kuwa Mali hizo baada ya kukabidhiwa kutoka kwa DPP zinakuwa chini ya uangalizi wa wizara ya fedha zinapangwa kadri serikali itakavyoona inafaa.
“Mali hizi Mara baada ya kukabidhiwa serikalini zitapangiwa matumizi kadri serikali itakavyoona inafaa na kama itaonekana Mali hizo hazifai kwa matumizi ya serikali zitauzwa kwa mnada” Alisema Rutha.
Kwa upande wake kamishina msaidizi wa jeshi la Polisi ,Selemani Nyakulinga Alisema Alisema kuwa mwaka 2011 alipata taarifa kutoka kitengo cha udhibiti wa fedha haramu kuwa kuna watu waligushi na kutaka kuiba fedha dolla la marekani milioni 17.2 kutoka mfuko wa global fund kwa ajili ya kusaidia kutibu malaria na HIV Nchini Tanzania zikitoka kwenye Hazina ya nchi ya Marekani.
Alisema walibaini kuwa waliohusika na wizi huo ni RAIA wa Kenya wakishirikiana na watanzania akiwemo Wakili Median Mwale .
Alisema baada ya kufuatilia walifanikiwa kuwatia mbaroni wahusika wote na baadae mahakama ilibaini kuwa wahusika walishanunua Mali mbalimbali zilizotokana na zao la utakatishaji wa fedha hizo na mahakama iliamuti na kutaifisha Mali hizo kuwa mali za serikali. 
Tags: UTAKATISHAJI FEDHAWAKILI MWALE
ADVERTISEMENT
I am Magnifico

I am Magnifico

Related Posts

Serikali kujenga vyuo vipya 33 vya VETA
HABARI TANZANIA

Serikali kujenga vyuo vipya 33 vya VETA

by Ombeni Osward
Jan 18, 2021
0

Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania...

Read more
RC Dodoma aongoza wenzake kwenye zoezi la upandaji miti

RC Dodoma aongoza wenzake kwenye zoezi la upandaji miti

Jan 18, 2021
Hospitali ya Bugando yakabiliwa na uhaba wa fedha

Hospitali ya Bugando yakabiliwa na uhaba wa fedha

Jan 18, 2021
Askari watakaoshinwa kubaini Wahamiaji haramu kuwajibishwa

Askari watakaoshinwa kubaini Wahamiaji haramu kuwajibishwa

Jan 18, 2021
Watumishi na taasisi za Umma wabanwa kulipa Kodi ya Ardhi

Watumishi na taasisi za Umma wabanwa kulipa Kodi ya Ardhi

Jan 18, 2021
Dkt. Gwajima Akemea vikali Ubadhirifu wa Dawa

Waliohusika na wizi wa Dawa kuchukuliwa hatua

Jan 17, 2021
Next Post

EBOLA YAUA ZAIDI YA WATU 1000 CONGO DRC

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

I agree to the Terms & Conditions and Privacy Policy.

Currently Playing

KRANTZ MWANTEPELE (FOUNDER & CEO)

ADVERTISEMENT

KONCEPT TV

https://www.youtube.com/watch?v=0HP0mB_rtIU&t=7s
ADVERTISEMENT
Mwanaharakati Mzalendo

Mwanaharakati Mzalendo ni mtandao namba moja kwa habari makini kutoka pande zote za dunia kuhusiana na Michezo, Siasa, Afya, Elimu, Mahusiano, Vituko, n.k

Wasiliana nasi kwa Email;krantzcharles@gmail.com
SIMU; 0658123310

Follow Us

May 2019
M T W T F S S
« Apr   Jun »
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
2728293031  
Currently Playing
  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

Login to your account below

Forgotten Password?

Fill the forms bellow to register

*By registering into our website, you agree to the Terms & Conditions and Privacy Policy.
All fields are required. Log In

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In