Mwanaharakati Mzalendo

BENKI YA DUNIA: MAZINGIRA YA BIASHARA TANZANIA YAZIDI KUWA MABAYA

Bwana Yutaka Yoshino kutoka Benki ya dunia
Mazingira ya biashara katika nchi ya Tanzania yametajwa kuongezeka kuwa mabaya zaidi katika miaka ya karibuni ukilinganisha na miaka ya nyuma huku sekta binafsi ikikandamizwa na kutopewa ushirikiano mzuri katika shughuli zao. 
Hayo yaliongelewa na wawakilishi wa Benki ya dunia ambao wamekuwa wakiufuatilia uchumi wa taifa hili kwa muda sasa na kugundua tatizo hilo ambalo ni kikwazo kwa uchumi wa viwanda inaoutaka. 
“Asilimia 97% ya ajira zote Tanzania hutokana na sekta binafsi na asilimia 89% ya bidhaa za viwandani pia ni kutoka sekta binafsi”- Mr. Yutaka Yoshino kutoka WB Public Private Dialogue. 
“Mazingira ya kufanya biashara nchini Tanzania yameporomoka kwa nafasi 12 kwa miaka 2 iliyopita. Si kwamba haifanyi mageuzi (reforms), bali ni kwa sababu washindani wake wanafanya mageuzi kwa haraka zaidi kuliko Tanzania.” Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia nchini, Bella Bird. 
Sekta binafsi Tanzania: 
*86% ya taasisi mbalimbali (shule, hospitali) ni za sekta binafsi.
*97% ya ajira zote nchini zinatokana na sekta binafsi.
*89% ya bidhaa za viwandani na 95% ya bidhaa zilizoongezewa thamani, zinazalishwa ba sekta binafsi. 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *