Mwanaharakati Mzalendo

BARABARA ZAFUNGWA MOSHI, WANANCHI WAFURIKA KANISANI IBADA MAZISHI YA MENGI

Umati umefulika katika ibada ya mazishi ya aliyekuwa Mwenyekiti wa Kampuni za IPP, Reginald Mengi.Barabara zote za kuingia na kutoka katika Kanisa Kuu la Usharika wa Moshi mjini wa Dayosisi ya Kaskazini ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), zimefungwa kwa kuwekewa utepe wa njano na polisi.

Hadi saa 3:30 asubuhi, kanisa lilikuwa limefurika waombolezaji ndani na nje kwenye mahema huku waombolezaji wengi wakifuatilia ibada hiyo nje ya uzio wa kanisa na eneo la mita za mraba 100 kuzunguka kanisa hilo.

“Sijawahi kuona umati mkubwa kiasi hiki katika kanisa letu. Hii inadhihirisha mzee Mengi aliishi kwenye mioyo ya Watanzania,” alisema Davis Mosha aliyewahi kugombea Ubunge Jimbo la Moshi mwaka 2015.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *