Mwanaharakati Mzalendo

KODI KUBWA YAWA CHANZO CHA WAFANYABIASHARA 116 KUFUNGA MADUKA TANDIKA

Biashara kufungwa
Katibu wa Wafanyabiashara mtaa wa Tandika esema kuwa Wafanyabiashara wamefunga maduka kwa kuhofia kuporwa maduka kutokana na ahadi aliyoitoa Mkurugenzi Jumatatu ya tarehe 12/05 mwaka huu kuwa kuanzia Jumanne siku ya pili yake atatuma watu waje wachukue kodi ambayo Katibu amedai haipo kisheria
Amesema kuwa alisema atakuja kuchukua kodi ya miezi mitatu ambao inaanzia laki 6 kwenda juu wakati kwa sasa ni laki na nusu. Lakini tulipo hoji kwanini wakati kodi hiyo sehemu nyingine inafika hadi elfu 70 akasema yeye anachukua kodi aitakayo
Amesema katika kikao hivho walichofanya na Mkurugenzi huyo baada ya watu kuhoji sana wakitaka kujua kodi hiyo ni ya nini na ipo vipi kisheria akaanza kuwa mkali na kuwaona watu wanaohoji ni Wavunja sheria baada ya hapo tukaona hali imekuwa tete
Aidha, Mwenyekiti wa Mtaa wa Tandika, Hassan Seif Shaa amesema Wafanyabiashara katika mtaa wa Tandika katika eneo la shule ya msingi Tandika wana masikitiko tangu mwaka 2010 ambapo ulipelekwa Waraka kuwa maduka hayo yavunjwe ila yalibadki baada ya mazungumzo ya muda mrefu
Amesema “Kwa yaliyowakuta Wafanyabiashara hivi sasa Mkurugenzi hakuishirikisha ofisini yake na yeye ameelewa malalamiko ya wafanyabiahara hao kupitia barua waliyoiandika kwenda kwa Mkurugenzi”
Aidha ameongeza kuwa ili kuimarisha kodi na kuzipata kwa wakati inabidi uongozi ukae na Wafanyabiashara ametolea mfano kuwa zamani soko la Temeke pekee lilikuwa linatoa kodi karibia Milioni 105 lakini sasa Masoko matano yanatoa Milioni 88 kwa ujumla
Mfanyabiashara mmoja amesema kuwa wao wameingia mkataba na shule ya Tandika na Mkurugenzi hataki kufuata mikataba iliyopo kisheria kwa maana anataka kivunja mikataba hiyo
Pia ameeleza kuwa kiwango cha kodi ambacho anataka kuchukua si rafiki hata kama ingekuwa halali lakini si rafiki. 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *