![]() |
Rammy Gallis |
Hivi karibuni akizungumza na gazeti la dimba, Rammy alisema kwa hadhi yake hawezi kufanya kitendo cha namna hiyo na hataki kuwa na mwanamke ambaye hajielewi kwa kushindwa kulea mtoto pale anaposhindwa kutoa huduma.
“Mimi nina jina kubwa sana kupitia kazi zangu, sasa inapofika hatua mtu anakudhalilisha kwa kudai una mtoto wake halafu hutaki kumlea, kwangu ni kunichafua na siwezi kuwa na mahusiano na mwanamke asiyejimudu kulea mtoto hata pale mimi ninapokwama kifedha,” alisema Rammy.
Hata hivyo, Gallis, ameiomba Serikali kuzingatia sheria za wanaume wanaokataa kulea watoto wao kwa kisingizio cha kutofunga nao ndoa na badala yake ametaka sheria hiyo ikaziwe na kuongezwa makali zaidi ili iwe fundisho.