Mwanaharakati Mzalendo

Tetesi za Soka Ulaya Leo Jumanne : Ramos, Sarri, Neymar, Dybala, Barcelona, Lo Celso, Gomes


Mchezaji wa Real Madrid na timu ya taifa ya Hispania, Sergio Ramos mwenye umri wa miaka 33 amemwomba bosi wa Real Madrid Florentino Perez kumruhusu aikache klabu yake na kwenda China. (LaSexta – in Spanish)Bosi wa Chelsea Maurizio Sarri ambaye amehusishwa kwenda kujiunga na klabu ya Juventus inasemekana kuwa amefikia makubaliano ya kupewa mshahara wa kiasi cha pauni milioni 1.2kila mwaka . (Mail)


Meneja wa timu ya taifa ya Uholanzi Ronald Koeman, Kocha wa zamani wa Juventus Massimiliano Allegri na Kocha wa Arsenal Unai Emery ni miongoni mwa watu ambao wanapewa nafasi ya kwenda kuchukua mikoba ya bosi wa sasa wa Barcelona Ernesto Valverd . (Mundo Deportivo – in Spanish)


Wakati huohuo taarifa zinasema kuwa meneja wa Ubelgiji Roberto Martinez ndie anapewa kipaumbele cha kwanza kuwa kocha mpya wa Barcelona kama Ernesto Valverde hataendelea na mkataba wake. (RAC 1 – in Spanish)


Mshambuliaji wa Juventus, Paulo Dybala mwenye miaka 25 amethibitisha kutaka kusalia na vibibi vizee vya Turin katika ya msimu ujao, licha ya kudaiwa kuwa anahitajika Manchester United. (Independent)


Arsenal tayari wamewasiliana na AC Milan kuhusu kusajili mlinda mlango wa Italia, Gianluigi Donnarumma 20. (Tutto Mercato Web via Star)
Real Madrid inalazima kumlipe mshambuliaji wa klabu ya Paris St-Germain Neymar mshahara wa pauni milioni 1.2 kwa wiki ili kuweza kumpeleka katika viunga vya Bernabeu. (AS via Mail)


Real Madrid wanahitaji kuongeza euro 300 kwa wachezaji wake katika msimu huu wa kiangazi. (Marca)


Mshambuliaji wa Eintracht Frankfurt’s Serbia Luka Jovic, 21 anaamini kuwa ligi kuu itafungua fursa kwake kupiga hatua . (Die Welt via Mirror)


Manchester United na Real Madrid zinaweza kumuwania mchezaji wa Argentina Giovani lo Celso, 23, msimu huu.


Mchezaji wa Ajax, Matthijs de Ligt, 19 amesema kwamba ripoti zinazomuhusisha kutaka kuhamia Manchester United zisizingatiwe.


Klabu ya West Ham iliweka kiasi cha pauni milioni 18 ili kupata saini ya kiungo wa kati wa Ureno Andre Gomes, 25 ambayo imekataliwa na Barcelona.


Miamba hawa wa Hispania wanataka kiasi cha pauni milioni 25 mpaka 35. (Sky Sports)


Swansea City imekubali kumuachia mchezaji wa kimataifa wa Wales Daniel James, 21 kwenda Manchester united kwa pauni milioni 15. (Manchester Evening News)


Mchezaji wa zamani wa Bayern Munich Lothar Matthaus ana uhakika kuwa mchezaji wa Manchester City kutoka Ujerumani Leroy Sane, 23, atajiunga na Bayern Munich msimu huu. (Sky Sports – in German)


Meneja wa Burnley Sean Dyche amedai kupata msukumo mkubwa wa kuuza wachezaji wake kipindi hiki cha kiangazi. (Lancashire Telegraph)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *