Mwanaharakati Mzalendo

Tetesi za Soka Ulaya Leo Alhamisi:Terry, Lukaku, Cancelo, Trippier, Rakitic, Wan-Bissaka

Nahodha wa zamani wa England na Chelsea John Terry, ambaye kwa sasa ni naibu meneja wa Aston Villa, anashauriana na Middlesbrough kuhusu uwezekano wa kuwa maneja wao mpya.(Talksport)Manchester City wanakaribia kumsajili beki wa Ureno Joao Cancelo, 24, ambaye thamani yake inakadiriwa na Juventus kuwa euro milioni 60. (Record – in Portuguese)


Atletico Madrid na Napoli wanapania kumsajili beki wa kulia wa Tottenham na mchezaji wa kimataifa wa England Kieran Tripper, 28. (Mirror)


Spurs wameweka dau la £10m kumnunua winga wa Leeds United wa miaka 18, Muingereza Jack Clarke. (Mail)


Manchester United wanashughulikia mpango wa kumsaini Ivan Rakitic, 31, lakini Barcelona wanataka kulipwa uero milioni 48 kumwachilia nyota huyo wa kimataifa wa Croatia. (Record)


United wanatarajiwa kuwasilisha dau la kwanza la £25m kumunua beki wa Crystal Palace, Aaron Wan-Bissaka, 21, lakini Eagles wanataka £50m kumwachilia mchezaji huyo. (Evening Standard)


Muargentina Sergio Romero, 32, huenda akapandishwa cheo kuwa kipa wa Manchester United ikiwa David de Gea, 28, ataondoka Old Trafford msimu huu wa joto. (Mail)


United tayari wamewasilisha rasmi ofa ya kumnunua kiungo wa kati wa Newcastle Sean Longstaff, 21. (ESPN)


Everton, West Ham na Manchester United wamepewa nafasi ya kumsaini kwa mkopo kiungo wa kati wa Uholanzi na Marseille Kevin Strootman, 29. (Sky Sports)


Antonio Conte anatarajiwa kusajili mshambuliaji wa Ubelgiji Romelu Lukaku, 26, kutoka Manchester United atakapoajiriwa kama meneja wa Inter Milan. (Times – subscription required)


Liverpool wanakaribia kukamilisha mpangowa £200,000 wa kumsajili kipa raia wa Poland Jakub Ojrzynski, 16, kutoka Legia Warsaw. (Liverpool Echo)


Wolves wanaongoza kinyang’anyiro cha kumsaini mshambuliaji Moussa Marega, 28 rai wa Mali ambaye thamani yake inakadiriwa kuwa £30m-kutoka Porto. (Mirror)


Newcastle, Southampton na Brighton wote wanataka kusaini winga Harry Wilson, 22, lakini Liverpool wanataka kulipwa £25m kumwachilia nyota huyo wa kimataifa wa Wales. (Sky Sports)


Bournemouth wako tayari kupokea ofa ya kummuuza winga Jordon Ibe, 23 raia wa Uingereza. (Mirror)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *