Mwanaharakati Mzalendo

WAKURUGENZI BUKOBA WAKAMATWA KWA KUTOA ZAWADI HEWA MEI MOSI

Mkuu wa Wilaya ya Karagwe ameliagiza Jeshi la Polisi kuwaweka chini ya ulinzi Kaimu Mkurugenzi Manispaa ya Bukoba, Josephat Kyebyera na Kaimu Mkurugenzi Halmashauri ya Bukoba, Siima Kyamani kwa kutoa zawadi hewa kwa wafanyakazi bora katika halmashauri zao
Mheluka aliyekuwa akimwakilisha Mkuu wa Mkoa Kagera katika maadhimisho ya sherehe za wafanyakazi (Mei Mosi), Mkoani humo, alimhoji Kyebyera iwapo amewapa zawadi wafanyakazi bora wa Halmashauri ya Bukoba aliokuwa amewaainisha na katika kujibu swali hilo, Kyebyera alisema zawadi zao za fedha tayari wameshawekewa kwenye akaunti zao za benki kama ilivyotakiwa na Serikali.
Walipoitwa wafanyakazi hao na kuulizwa iwapo kuna yeyote amewekewa fedha zake kwenye akaunti yake, wote walikataa na kusema hawajaingiziwa fedha hata shilingi moja. 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *