Amber Lulu amedai Shilole ambaye ni dada yake amekua akimshauri mengi na yeye akiwa mdogo wake anatamani kumuona na mwili wake wa zamani kwa kuwa ulikua unampa mwonekano mzuri zaidi ya sasa.
“Shilole ni dada yangu, amekua akinishauri hata kazi zangu za muziki, na mimi kama mdogo wake ikifika sehemu ya kumshauri natumia nafasi yangu, ni kweli kwa sasa ameongezeka mwili sana na natamani arudi kama awali kwani hapendezi” alisema Amber Lulu.
Msanii huyo kwa sasa ameachia ngoma mpya inayokwenda kwa jina la Machozi ambayo inafanya vizuri akiwa kamshirikisha Marioo.