Mwanaharakati Mzalendo

DJ KHALED APANGA KUWABURUZA MAHAKAMANI BILLBOARDS, SABABU HIZI HAPA

DJ Khaled alitumia kiasi cha $5 million sawa na Tsh Bilioni 12 kuitayarisha tu album yake mpya ya ‘Father Of Asahd’. 
Hii huenda ikawa ni sababu kubwa ya kupanga kuwaburuza mahakamani Billboard kwa album yake kushindwa kukamata namba 1 kwenye chati za Billboard 200 wiki moja baada ya kuachiwa rasmi. 
Sababu ya Khaled kuipeleka kortini Billboard ni kushindwa kuchukua mahesabu (100,000 Units) ya mauzo ya nguo “Merch” za album hiyo kama walivyofanya kwa “IGOR” ya Taylor The Creator ambayo ilikamata namba 1. 
Kama ulikuwa haufahamu, Billboard wanahesabu na mauzo ya bidhaa za nguo (Merchandise Sales) na kuyaweka kwenye mjumuisho wa mauzo ya nakala za album. 
Hii inaturudisha kwenye ugomvi wa albamu ya Nicki Minaj (QUEEN) na Travis Scott (AstroWorld) mwaka jana ambapo yaliwakuta pia. 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *