Mapema leo ligi kuu ya Uingereza maarufu kama EPL, imetoa ratiba za mechi zote za msimu ujao wa 2019/2020 na kuonyesha kuwa ligi hiyo itaanza ijumaa ya tarehe 9 mwezi AUGUST mwaka huu kwa mchezo mmoja pekee kati ya Liverpool Vs Norwich city.
Siku ya jumamosi ndio itakayokuwa na mechi nyingi sana huku jumapili kukiwa na mechi kali 2. Moja itakutanisha kati ya Mashetani wekundu Manchester United Vs Chelsea na nyingine Vijana wa Rafa Benitez Newcastle watawavaa Arsenal ya Unai Emery: