Mwanaharakati Mzalendo

INDIA YAONGEZA USHURU KWA BIDHAA ZA MAREKANI

Wizara ya fedha ya India imetoa taarifa kuwa serikali yake imeamua kuongeza ushuru kwa bidhaa 28 zinazoagizwa kutoka Marekani zikiwemo lozi, maharagwe na walnut kuanzia tarehe 16 mwezi huu. 
Mwezi Juni mwaka jana India ilianza kuandaa orodha hii ya bidhaa za Marekani zinazoweza kuongeza ushuru, ili kulipiza kisasi kutokana na Marekani kuongeza ushuru wa chuma na aluminium zinazoagizwa kutoka India. 
Hapo awali India iliahirisha muda wa kuongeza ushuru wa bidhaa hizo, ili kuhimiza mazungumzo husika na Marekani. Lakini June 5 mwaka huu serikali ya Marekani ilitangaza kuiondoa India kutoka kwenye Mfumo wa Upendeleo GSP kwa kuwa India haitoi soko la haki na wazi kwa Marekani, na kusababisha uhusiano wa kibiashara kati ya nchi hizo mbili kuwa mbaya zaidi. 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *